Friday, 3 August 2007

TUT inatumia vibaya pesa za walipa kodi - MOAT

03 Aug 2007By Lucy Lyatuu, Dodoma
Taarifa ya Media Owners Association of Tanzania (MOAT) kwa vyombo vya habari kuhusu Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT) kujiingiza kwenye matangazo ya biashara. Televisheni ya Taifa (TvT) na Radio Tanzania (RTD) zinafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali kupitia fedha za walipa kodi. Watangazaji Binafsi hulipa gharama nyingi zikiwepo malipo ya masafa, leseni, kodi za mapato na nyinginezo. Malipo haya kwa njia moja au nyingine yanachangia ufadhili wa TvT na RTD. Kwa sababu hii TvT na RTD hazina haki zozote zile za kushindana na Watangazaji Binafsi katika mapato yatokanayo na matangazo ya biashara. Ushindani huu usio halali unazidi kuwa mbaya zaidi pale TvT na RTD wanapotoza ada yoyote wanayopenda kwa matangazo ya biashara, tena ikiwa ni kidogo mno kulinganisha na ada zinazotozwa na Watangazaji Binafsi. TvT na RTD zina uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu hazijiendeshi kwa gharama zao, hazipati hasara. Kwa kutoza ada kidogo, wanateka soko la Watangazaji Binafsi na kwa sababu hiyo kuwadhoofisha kiuchumi. Mwenendo huu unalenga kuwaua kiuchumi Watangazaji Binafsi ambao wanalipa kodi zinazozifadhili TvT na RTD. Matangazo na maonyesho ya kibiashara ya TvT na RTD yanasikitisha sana Watangazaji Binafsi. Yanadhoofisha jitihada zao za mikakati ya biashara kwa kuingiza ushindani usio halali na yanaathiri vibaya uwezo wa soko ambalo limeanzishwa na kukuzwa kwa gharama kubwa na Watangazaji Binafsi. Hivi karibuni Taasisi ya Utangazaji (TUT) imeonyesha dhamira yake ya kuvamia utangazaji wa kibiashara wa mashindano ya mpira wa miguu. Ili kufanikisha lengo hili TUT imekuwa inalipa fedha nyingi sana za walipa kodi kuwapiku Watangazaji Binafsi katika kununua haki pekee za kutangaza na kuonyesha mashindano hayo. Kwa mfano:TUT ililipa takriban Tsh. 265.0 millioni kununua haki pekee za kutangaza Ligi Kuu ya Uingereza. Watangazaji Binafsi walikuwa wamependekeza kiasi cha takriban Tsh. 105.0 milioni ambazo zingeweza kukubalika kama TUT wasingekuwa wamelipa kiasi hicho kikubwa cha fedha. Kwa vile dau la juu zaidi kitaifa ndilo linaloshinda haki hizo, TUT bado ingeweza kushinda kwa kulipa fedha kidogo tu juu ya dau la juu zaidi lililopendekezwa na Watangazaji Binafsi. Ni vigumu kuamini kwamba fedha nyingi namna hiyo za walipa kodi ziliweza kutupwa ovyo na TUT pasipo kujali hata kidogo. Watangazaji Binafsi walikuwa na nia ya kutangaza mechi ijayo kati ya Msumbiji na Taifa Stars na walipendekeza malipo ya kati ya Tsh. 14.0 na 15.0 milioni. Haki za kutangaza mchezo huo zilinunuliwa na TUT kwa Tsh. 27.0 milioni na kwa mara nyingine tena kuwapiku watangazaji binafsi. Katika tenda zote hizi, TUT ilitumia vibaya fedha za umma kujipatia ushindani usio halali dhidi ya Watangazaji Binafsi. Mwenendo huu unaashiria kwamba huko tuendako, Watangazaji Binafsi kamwe hawatapata fursa ya kutangaza/kuonyesha mashindano makubwa ya mpira wa miguu kama TUT itaendelea kuruhusiwa kutumia bila kujali fedha za walipa kodi ili mradi imewapiku Watangazaji Binafsi katika matangazo ya aina hii. Na kwa kutumia njia hii, TUT itakuwa imewezeshwa kikamilifu kuzuia mapato yanayotokana na chanzo hiki kwa Watangazaji Binafsi. MOAT inahisi kwamba TUT imeagizwa au imepewa mamlaka na ofisa au maofisa wa ngazi ya juu Serikalini kushindana vikali na Watangazaji Binafsi kwa gharama yoyote ile, na kwa kusudio hilo inapewa fedha nyingi kufanikisha kazi hiyo. Ni lazima ieleweke kwamba programu za Watangazaji Binafsi zinatia maanani pia masuala ya maendeleo ya ustawi wa jamii na kwamba Watangazaji Binafsi wanatumia sehemu kubwa ya mapato yao kugharamia programu hizo, hasa ukusanyaji wa habari. Inapaswa pia ieleweke kwamba iwapo mapato ya Watangazaji Binafsi yatadhoofishwa kwa kutumia njia hii ya ushindani usio halali, Watangazaji Binafsi watashindwa kuunda na kusambaza programu hizo kikamilifu na kwa ufanisi uliotarajiwa. Kwa maoni ya MOAT, TvT na RTD kama Watangazaji wa umma zinapaswa kujishughulisha na utangazaji wa masuala muhimu ya umma tu na kuacha kabisa kushughulika na matangazao ya biashara. MOAT inaiomba Serikali kutambua mchango mkubwa wa Watangazaji Binafsi katika maendeleo ya jamii na kuhakikisha kwamba mazingira ya shughuli zao yanawezesha upatikanaji wa mapato yanayotosheleza gharama zao na kuchangia pato la taifa. Hususan, Serikali isiunge mkono shughuli za ushindani usio halali ambao hatimaye utawauwa kifedha Watangazaji Binafsi. MOAT ina imani kwamba Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania italishughulikia suala hili ambalo linawagusa sana Watangazaji Binafsi ili kuhakikisha kwamba Watangazaji Binafsi wanalindwa dhidi ya tishio hili kubwa la ushindani usio halali.
* SOURCE: Nipashe

No comments: