Friday, 10 August 2007

Umbea, unafiki na majungu ndani ya Reading!!!

Kufuatia habari na matangazo kuwa African Stars wanatarajiwa kufanya ziara London, Uingereza hivi karibuni, mdau mmoja mkazi wa mji wa Reading ametoa wito kwa waandaaji wa maonesho ya Twanga pepeta kuwa wafike pia Reading kutoa burudani:
'London pekee haitoshi, waje pia Reading kuna washabiki kibao!'

Wadau wa LONDON wamjibu mdau wa Reading:
Tarehe August 9, 2007 11:24:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
hello, anon wa 11:36 Twanga pepeta wataishia London, usiwashushe hadhi, hawawezi kuja Reading, huko ni Uswahilini sana,,nasikia kuko kama Manzese tu, umbea, udaku, kusutana, kuibiana mabwana na mabibi n.k nasikia mpaka kurogana pia,shuti kwa waganga wa kigambia eti,,mmh,,kila la kheri na hivi ticket za bongo sikuhizi bei chee, Qatar airways..mh mtakuwa mnawafuata waganga wa jadi , kama walioko Reading hawawatoshi.

Tarehe August 9, 2007 11:28:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
Reading ndio nini? aah, kule Manzese kwa mfuga mbwa eeh, ooh kweli lazima washabiki muWe wengi, kwa maana wote waswahili tu, shule hammalizi, nyumbani hamuwezi kurudi kuwasabahi ndugu zenu,,mmeshakuwa Big brother Reading, mikoba mmeichoma moto, MMEJILIPUA, Ufuateni Mugongomgongo London, KAMA MNAYO NAULI....

source: issamichuzi blog

No comments: