Monday, 6 August 2007

Dar: Nauli za daladala zatangazwa

Nauli halisi za daladala Dar zatangazwa
Ni za kulipa kulingana na umbali Kariakoo-Mbagala,
ubungo vyarudi vya zamani
Mwenge-Posta, Kariakoo vyaongezeka kwa sh. 100
Na LEON BAHATI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza viwango halisi vya nauli za daladala mkoa wa Dar es Salaam.Viwango hivyo vinaanza kutumika kuanzia wiki hii ambapo uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya njia zitatoza nauli ya zamani wakati ambapo baadhi ziomeongezeka kwa kati ya sh. 50 na 300.Viwango hivyo vitakuwa vimefuta utaratibu uliotangazwa awali kwamba nauli ya njia zote itaongezeka kwa sh. 50. Meneja uhusiano wa SUMATRA, Devid Mziray aliliambia Uhuru mwishoni mwa wiki kuwa viwango hivyo vipya vimepangwa kulingana na umbali wa kituo hadi kituo.
Mnziray alisema kuwa umbali kati ya kilomita :
0-10 ni sh. 250,
11-15 sh. 300,
16-20 sh. 350,
21-25 sh. 400,
26-31 sh. 500 na
32-40 sh. 600.
Baadhi ya abiria watakaofaidika na viwango hivyo vipya ni wa njia ya
Ubungo-Kariakoo, Ubungo-Posta, Mbagala-Kariakoo, Mbagala-Stesheni ambao watalipa viwango vya zamani vya sh. 300.
Hata hivyo, Uhuru limebaini kuwa abiria wa njia hizo kwa sasa wanatozwa sh. 350 bila kujali vituo walivyoanzia safari ama mwisho wa safari.
Nauli hizo mpya zinaonyesha kuwa nauli ya Mwenge-Kariakoo, Posta na Kivukoni zimeongezeka kwa sh. 100 ambapo sasa itabidi walipe sh. 300 badala ya 200 ya zamani.

Nauli mpya ni kama zifuatazo:
Mbagala-Mivinjeni sh. 250,
Mbagala-Bandari sh. 300,
Mbagala-Kariakoo sh. 300,
Mbagala-Akibaza sh. 300,
Mbagala-Posta-Kivukoni sh. 350.
Kivukoni-Uhasibu sh. 250,
Kivukoni-Mtoni Kwa Azizi Ally sh. 300,
Kivukoni-Mbagala Mission 300,
Kivukoni-Mbagala Kizuiani-Mbagala 350.
Kibamba-Kariakoo sh. 500,
Kibamba-Kimara sh. 300,
Kibamba-Ubungo sh. 350,
Kibamba-Shikilango sh. 300,
Kibamba-Manzese-Magomeni sh. 400,
Kibamba-Muhimbili sh. 500.
Kimara Mwisho-Posta-Kivukoni sh. 350,
Kimara-Kariakoo sh. 300,
Ubungo-Posta sh. 250,
Ubungo-Kivukoni 300,
Manzese-Posta-Kivukoni sh. 250 na
Ubungo-Kariakoo sh. 250.

Mwenge-Posta,
Mwenge-Kariakoo, Mwenge-Kivukoni zote watalipa sh. 300,
Mwenge-Fire sh.250,
Kivukoni-Mwananyamala 250,
Kariakoo-Bamaga sh. 250,
Mwenge-Manzese sh. 250 na
Kivukoni-Shekilango 250,

Mwenge-Sinza 250,
Sinza-Posta 250
Sinza-Kariakoo sh. 250 na
Sinza-Kivukoni sh. 300.

Tegeta-Kariakoo sh. 400,
Tegeta-Posta-Kivukoni sh. 500,
Tegeta-Mwenge sh. 300,
Tegeta-Njiapanda Kawe sh. 300,
Tegeta-Mwananyamala sh. 350,
Tegeta-Mabibo sh. 400 na
Tegeta-Njiapanda Mabibo sh. 350,

Tegeta-Mbagala sh. 600,
Tegeta-Magomeni sh. 400,
Tegeta-Kigogo Mbuyuni 400 na
Tegeta-Temeka 600.

Gongolamboto-Kariakoo-Mnazimmoja-Akiba sh. 300,
Gongolamboto-Posta-Kivukoni sh. 350,
Gongolamboto-Tazara 250,
Uwanja wa ndege-Posta-Kivukoni sh. 300,
Vingunguti-Posta 250,
Vingunguti-Kivukoni 300,
Tazara-Kariakoo na Posta sh. 250,
Kivukoni-Majumbasita sh. 300 na
Kivukoni-Tazara 250.

Tabata Segerea-Kivukoni sh. 350,
Tabata Segerea-Kivukoni-Posta sh. 350,
Tabata Segerea-Kariakoo-Mnazimmoja sh. 300,
Tabata Segerea-Rozana 250,
Tabata Segerea-Stesheni sh. 300,
Tabata Segerea-Temeke sh. 300,
Tabata Segerea-Tandika kupitia Everet sh. 350 na
Tabata Segerea-Buguruni sh. 250.

Tabata Kimanga-Mnazimmoja-Kivukoni sh. 300,
Tabata Kimanga-Mchikichini sh. 250,
Kivukoni-Rozana sh. 250,
Kivukoni-Tabata Relini sh. 300,
Tabata Kimanga-Stesheni 300,
Tabata Kimanga-Temeke sh. 300 na
Tabata Kimanga-Ubungo sh. 250.

Kigogo-Muhimbili 250,
Mwananyamala-Muhimbili 250,
Mwananyamala-Kariakoo 250,
Mabibo-Kivukoni 250,
Mabibo-Kariakoo 250 na
Mabibo-Muhimbili 250.

Mziray alisema kuwa majedwali kwa ajili ya njia nyingine hususani za pembezoni mwa jiji zitatangazwa mara maandalizi yake yatakapokamilika.Alisema kuwa kila daladala inapaswa kuwa na jedwali la nauli kulingana na njia kinakofanya kazi na kwamba msako mkali utafanywa baadae mwezi huu ili kuwatia mbaroni watakaokuwa hawajatekeleza amri hiyo.
Wakosa makazi baada ya nyumba kuteketea motoNa Scolastica Komba, BagamoyoWAKAZI 92 wa kijiji cha Kifleta, kata ya Mbwewe, wilayani Bagamoyo hawana makazi kutokana na nyumba 20 kuteketea kwa moto.Mkuu wa wilaya hiyo, Serenge Mrengo alisema moto huo ulioteketeza pia baadhi ya mashamba ulitokea mchana wa Julai 30, mwaka huu.Mrengo alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk. Christine Ishengoma aliyetembelea kijijini hapo kuangalia uharibifu uliotokea na kuwapa pole wanakijiji hao.Mrengo alisema chanzo cha moto huo ni majivu yaliyokuwa yamemwagwa shambani na mmoja wa wanakijiji hao yakiwa bado yana moto. Alisema kutokana na upepo, moto huo uliruka kwenye nyasi kavu na kusambaa. Mkuu wa wilaya alisema wakati moto huo ukiwaka, wakulima wengi walikuwa mashambani.Mrengo alisema moto huo uliunguza mashamba, maeneo ya misitu na kuunguza nyumba kutokana na nyingi kuzungukwa na nyasi. Alisema kijiji hicho kina kaya 18 na kwamba hadi sasa watu 92 hawana makazi, kati yao wanawake wakiwa 16, wanaume 16 na watoto 60, ambao wanaishi kwa majirani. Alisema hatua kadhaa zimechukuliwa kuwasaidia wananchi hao.Alisema nyumba tisa ndizo zilizosalimika kutokana na wakazi wake kuwepo wakati moto huo ukiwaka, hivyo kufanikiwa kuuzima.Mkuu huyo wa wilaya alisema hasara iliyotokana na moto huo ni sh. milioni 7.7. na kwamba mkulima Hussein Juma Boga (25), anayedaiwa kusababisha moto huo ametoweka kwa kuhofia kuchukuliwa hatua za kisheria.Dk. Christine aliwaomba wananchi kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia wanakijiji hao, kwani hawana nguo, vyakula na malazi. Pia alikema tabia ya kuwasha moto ovyo.

JK APOKEWA KWA KISHINDO ROMBO
Wananchi wafunga barabara
Asema wanaosema ccm itashindwa kutekeleza ahadi walie
Na mwandishi Maalumu, Rombo
RAIS Jakaya Kikwete amesema , serikali ya Chama Cha Mapinduzi itazitekeleza ahadi zote ilizowaahidi wananchi, na kwamba wale wanaosema itashindwa wao walie tu. Aliwahakikishia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wa hadhara alioufanya katika mji mdogo wa Tarakea, kuwa serikali yake imejiandaa kikamilifu kuzitekeleza ahadi hizo hatua kwa hatua kama ambavyo imeshaanza kuzitekeleza ahadi hizo.Rais ambaye aliwasili wilayani Rombo akitokea wilayani Mwanga, katika vijijini vyote alivyopita akielekea Tarakea alilakiwa na mamia ya wananchi waliofunga barabara wakimtaka asimame na kusalimiana naye nay eye akafanya hivyo.“Ndugu wananchi nimekuja kuwasalimia, kwanza nawashukuru kwa mapokezi makubwa ambayo hajawahi kutokea kote nilikowahi kufika. Nimekuja kuwashukuru kwa kutuchagua, tulikuwa wengi lakini mkasema mnamtaka Kikwete, vilikuwapo vyama vingi lakini mkasema mnaitaka CCM. Kwa hiyo nimekuja kuwashukuru. Na kuwaambia kwamba tutatekeleza kila tulichoahidi wakati wa kampeni na kwenye ilani ya CCM” alisema.Aliongeza; “ Wako wale wanaosema wakati wa kampeni tuliahidi mambo mengi lakini hatutawezi kuyatekeleza, lakini sisi tunatekeleza kile tulichokiahidi na tumeanza kazi hiyvo wao walie tu”.Katika wilaya hiyo ya Rombo ambako Rais alipokelewa na makundi ya watu huku wengine wakifunga njia na kumlazimisha asimame na kusalimia naye. Rais alisema ahadi ya kuitengeneza barabara ya kutoka Kiraracha kupitia Rombo Mkuu hadi Tarakea itakamilika na kwamba tayari mkandarasi amesha anza kazi.“Nimekuja kuwahakikishia kwamba hili vumbi mnaloliona kwenye barabara na kwenye mabati ya nyumba zetu, hili ni vumbi la mwisho, baada ya muda mfupi litakuwa limekwisha, kwa sababu mkandarasi ameshaanza kazi,” alisema Kikwete.Alisema kwamba katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga asilimia 75 ya bajeti yake kwa ajili ya ujenzi wa barabara nchini, kwa kuwa inatambua kwamba barabara ndiyo muhimili mkuu wa uchumi wa nchi.Kuhusu tatizo la maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo, Rais alisema ingawa serikali haina uwezo mkubwa lakini katika uwezo wake huo mdogo na kwa kushirikiana na marafiki mbalimbali duniani inaouwezo wa kufanya mengi ya kuboresha huduma muhimu na za msingi kwa maisha ya watanzania.Katika mkutano huo Rais pia aliwasisitiza wananchi kutoacha kupeleka watoto wao shule, kuendelea kujitolea katika ujenzi wa shule za sekondari, zahanati na vituo vya afya, lakini pia kujidhari dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.Akielezea zaidi kuhusu ukimwi ambao katika wilaya hiyo kiwango cha maambukizi ni asilimia saba, aliwata wananchi hao kuwa waangalifu na kujikinga na maambukizi na hasa kwa kuwa Tarakea ni kituo kikubwa cha biashara.

VIJANA WANAWEZA UONGOZI-JK
Akufurahishwa na utendaji wa mkuu wa wilaya Mwanga
Ataka wapewe fursa zaidi
Wazee wamwomba asimhamishe.
Na Mwandishi Maalumu,
MwangaRAIS Jakaya Kikwete amesema vijana wanaouwezo mkubwa wa kutekeleza kwa ukamilifu na umakini majukumu mbalimbali ya uongozi ili mradi wapewe fursa ya kufanya hivyo."Taarifa ya mkuu wenu wa wilaya imenipa faraja kubwa sana, wilaya yenu iko mbioni. Yeye ni kielelezo kwamba vijana wanaweza wakipewa fursa ya kuongoza, wenyewe mmeona mkuu wenu wa wilaya kazi anayoifanya. Nimefurahi sana " alisema Rais na kushangiliwa na wananchi.Alibainisha kwamba umahiri wa vijana katika utekelezaji wa majukumu yao, hauwezi kuonekana kama hawatapatiwa fursa na kusisitiza kwamba ili vijana waonekanae kwamba wanaweza ni lazima wapewe nafasi.Rais aliyasema hayo, wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika juzi katika uwanja wa michezo wa Cleopa David Msuya, mjini Mwanga ambako alikuwa na ziara ya kukagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo.Mkuu huyo wa Wilaya ya Mwanga, Jordan Rugimbana, ni kati ya wakuu wa wilaya vijana nchini, na aliteuliwa kuongoza wilaya hiyo mwaka 2005 hivi sasa ana miaka 38.Utendaji kazi wa mkuu huyo wa wilaya sio tu kwamba umemfurasha Rais Kikwete peke yake, hata wananchi wa wilaya hiyo wakiwamo wazee, wameelezea kuridhika kwao na kiongozi wao kiasi cha kumuomba Rais asimhamishe wilayani hapo."Mhe. Rais Rugimbana ameibadilisha wilaya yetu, tuachie usimuhamishe ili aendelee kuibadili wilaya ya Mwanga iwe Ulaya."Mkuu wetu wa Wilaya anashirikiana vizuri na kila mtu vijana kwa wazee ni mtiifu, anayeibua miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii, " usimhamishe Mhe. Rais ili aendelee kukamilisha kazi aliyoianza na aendelee kuibua miradi mipya na sisi tutampa ushirikiano," aliomba Mzee Abdallah.Katika mkutano huo wa hadhara, Rais aliwaeleza wananchi juhudi zanazofanywa na serikali za kuwapatia maji safi na salama ya kutosha wananchi wa Pare ya Tambarare."Kimsingi BADEA wamekubali kutusaidia katika mradi huu ambao ulikuwa mradi wangu wa kwanza kuwaomba wakati nilipokutana na Rais wa BADEA, ila sasa wamesema wataweza kutupatia dola za Marekani milioni 18 (zaidi ya sh. bilioni 20) na dola milioni 15 zitakazobaki ama tutoe wenyewe au tutafute wafadhili wengine, ndiyo kazi tunayoendelea nayo sasa, ahadi yetu ya kuwaondolea kero iko pale pale" alisema Rais Kikwete na kushangiliwa na wananchi.Ahadi nyingine kwa wilaya ya mwanga ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na kwamba kwa kuanzia zitajengwa kilomita 14 kutoka njia panda na nyingine zitaimarishwa ili ziweze kupitika kwa mwaka mzima.Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo, kwa Rais Kikwete mara tu baada ya kuwasili wilayani hapo akitokea wilaya ya Same, taarifa ambayo iliainisha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Mkuu huyo wa wilaya alimweleza Rais kwamba wilaya yake ni ya pili kitaifa kwa kufaulisha watoto wengi. Akijieleza kwa ufasaha na kujiamini, Rugimbana alisema wilaya yake ina shule za msingi 108, shule za awali 79, sekondari 35, vyuo viwili vya ufundi staid na chuo kimoja binafsi kunachofundisha walimu.Rugimbana alisema wilaya yake ina lengo la kuwa na zahanati 60, kwa sasa kuna zahanati 43 sawa na asilimia 72.Alisema katika uboreshaji wa huduma za afya, jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na uongozi wa wilaya pamoja na wananchi ni uanzishaji wa mfuko wa afya ya jamii, ukarabati wa zahanati na vituo vya afya na ujenzi wa vituo vya afya.Kuhusu ugonjwa wa ukimwi, mkuu huyo alisema, ugonjwa huo bado ni tatizo kubwa katika wilaya yake na kwmaba kiwango cha maambukizi kwa mwaka 2006 kilifikia asilimia tano.Akizungumzia hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya alimweleza Rais kwamba hali ni shwari kwa ujumla ingawa kumekuwapo na matukio ya mara kwa mara ya uhalifu ya wizi, unyang,anyi wa kutumia silaya na ajili za barabarani.Akiwa Wilayani Mwanga, Rais Jakaya Kikwete aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha afya Mwanga ambacho hadi kukamilika kwake kitagharimu sh. milioni 350 na na Rais akachangia sh. milioni tatu. Rais pia alifungua soko jipya na kufungua uwanja mpya wa michezo wa Cleopa David Msuya.

Uhuru

No comments: