Friday, 14 December 2007

Weupe!!!

Sio ajabu kukuta hali ya ubaguzi wa rangi ktk maeneo ya kazi na burudani Ulaya.

Amini usiamini kuna maeneo mengine ya kimaisha ambayo baadhi ya 'wazungu' wanawathamini watu weusi kuliko wazungu wenzao.

Ombaomba weupe/wazungu barabarani wanawaomba hela watu weusi zaidi kuliko kwa wenzao weupe. Kama mtu mweusi ameongozana na mzungu, utakuta mzungu anapita lakini ombaomba kimya! Lakini mtu mweusi akikaribia tu ombaomba anamsimamisha na kueleza shida yake! Aghalabu weusi husaidia ombaomba kuliko wazungu wenzao. Inaonekana ombaomba wazungu hawana kasumba ya ubaguzi au ni shida inawafanya waonekane marafiki wa weusi?

Pia kuna wazungu wanaoeneza injili njiani. Wakimwona mtu mweusi tu wanamchangamkia kwani wanajua weusi hujali na kusikiliza. Lakini huwa wanawakwepa wazungu wenzao! Kwa hiyo neno la Mungu linawaendea weusi. Hii ni POA!

Lakini ubaguzi bado upo, sidhani utaisha hivi karibuni. Maana hata wale wanaotoka nchi zenye shida kama zetu (ulaya mashariki) wakishafika Ulaya Magharibi wanatubagua weusi, wakati na wao ni shida imewaleta!

No comments: