Monday, 31 December 2007

Kila la Heri 2008

Ndugu na marafiki zangu,
Ni furaha iliyoje leo kufikia ukingoni mwa mwaka 2007!
Nikiwa bado nimejawa na hiyo furaha napenda pia kuwatakieni heri na mafanikio mema ktk mwaka mpya ujao 2008.
Wachumi wanatabiri kuwa utakuwa ni mwaka mchungu kiuchumi na kimaisha karibu sehemu zote duniani!
Maisha yatakuwa magumu na hela itakuwa ngumu kupatikana na hivyo kuongezea machungu na makali ktk hali tunayokabiliana nayo kwa sasa!
Ni matumaini yangu kuwa tutajiandaa kikamilifu kihali na kifikra ili kupunguza yale makali yatakayotuandama.
Bila shaka tukiungana -hasa ktk kusaidiana mawazo, mbinu na nyenzo za kimaisha tunaweza kufanikiwa.
Mungu awabariki sana!
Tukutane tena 2008 tukiwa wenye furaha na afya tele!!

No comments: