Tuesday, 11 December 2007

Kuporomosha Maghorofa!

Ipo dhana kwamba pale mtu anapofanikiwa kimaisha ni lazima ajenge nyumba ya/za ghorofa kama makazi yake, ili athibitishe uwezo wake kiuchumi katika jamii! Yaani mtu anahangaika kutafuta mali na hela ili siku moja aweze kujenga ghorofa!
Mara kadhaa utasikia maongezi mitaani, 'mwenzio keshajenga nyumba ya ghorofa ...!'

Naomba nieleweke kuwa sio dhambi wala makosa mtu kujijengea ghorofa. Lakini kinyume na fikira za wengi, nyumba za ghorofa hujengwa kwa sababu fulani na sio chaguo la moja kwa moja (automatic) pale unapokuwa na pesa. Uamuzi wa kujenga ghorofa waweza kutokana na uhaba au ufinyu wa eneo la kujenga vis-a-viz clients requirements etc.

Kuna aina kuu 2 za kuendeleza makazi ya kuishi (settlement planning):
1. kiubavubavu (horizontal extension)
2. Kwenda juu (vertical extension)
Mara nyingi zaidi horizontal expansion hupendelewa zaidi kwa sababu ni nafuu na rahisi kujenga.
Vertical extension ni ghali kwani gharama za ziada huongezeka kama vile scaffolding, stairs, hoisting (of materials etc.)

Ikumbukwe pia kuwa uwezo wa kifedha pekee sio kigezo tosha (kufikiria) kuporomosha maghorofa.

Kabla mtu hajaanza kuliporomosha, hata kama 'anazo' ningependa kushauri vitu* vya kufikiria kwanza:-
1. nini mahitaji yake (clients requirements - ukubwa wa familia yake ambao utasaidia kupanga mahitaji mengine + 'spatial analysis' za vyumba, vyoo, (ma)jiko n.k.
2. site analysis
3. matumizi ya jengo (ni la kuishi tu au ni pamoja na biashara?)
4. eneo analotaka kujenga (site location)
5. ukubwa wa eneo la kujenga (site size)
6. kuingilika kwa site (hasa katika kuingiza vifaa na mitambo kama itahitajika)
7. taratibu za serikali za mitaa husika - mipango miji, manispaa na majiji (by-laws -mambo kama plot ratio, masterplan n.k.)
8. majirani wamejengaje au vipi (nyumba za majirani ni za aina gani - context).

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo kwangu nayaona muhimu pale mtu anapopata uwezo wa kufanya kweli. Ukishapata majibu ya mambo hayo ndio utaweza kuwa katika nafasi ya kuamua ni nyumba ya aina gani utajenga ktk kiwanja chako.

Natoa ongezi kwa wale waliokwisha timiza ndoto zao tayari, na wale ambao wako mbioni nawatakia kila la heri. Cha msingi ni kujiuliza, je shida yako ni kujenga nyumba au kujenga ghorofa?


*ni rahisi kutekelezeka iwapo mtaalam atahusishwa ktk kuandaa na kuendeleza michoro.

No comments: