Thursday, 6 December 2007

TZ: Ni 'Mtakuja' au 'Imetoka hiyo, ikirudi ...'?

Yafuatayo ni maoni ya wa-TZ walioko nje na wa ndani ya nchi yetu kuhusu ya maisha ya nyumbani baada ya masomo/maisha nje ya nchi. Huu pia ni majadala. Shukurani toka lwa Michuzi Blog.
-Mosonga


Bro Michuzi,
Leo naomba niwakilishe mada nyeti na muhimu sana haswa ikiwagusa watanzania tulioko nje ya nchi na naamini kama watu wakiijadili kisawasawa basi wengi wetu hususan wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nje ya nchi tutaifaidi vilivyo na itaweza kutusaidia pale tunapotaka kufanya maamuzi muhimu ya maisha.

Mada: Je UKIMALIZA kusoma abroad (Specifically Bachelors, masters na Phd) URUDI nyumbani au UENDELEE na maisha abroad? Je ni kweli waweza lipwa au jilipa hela nzuri zaidi sawa au hata zaidi ya huku mamtoni? Je ni wangapi waliorudi wanafurahia maamuzi ya kurudi na kufanya kazi nyumbani? Je ni estimate ya dola ngapi kiwango cha chini makampuni Tanzania yatakulipa ukiwa na elimu kuanzia bachelors hivi??? hapa ni muhimu sana figure kamili zitajwe za mishahara watu tupate ka-idea!!

Akhsante,
Mdau mwakilishaji

© Michuzi Tarehe: 5.12.07 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |



54 Comments:



Tarehe Wednesday, December 5, 2007 9:56:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Binafsi, nimemaliza Masters Holland, I am happy kurudi nyumbani.
Sababu, huku home nafanya kazi ya professional yangu, tofauti na Holland ambako nilikuwa naosha vyombo hotelini na kusafisha Maua. Kwanza kazi ngumu, kusimama muda mrefu na huthaminiwi, wanaona kama umekosea kwenda kwao na wanakutumia vile vile.
Outings chache sababu kila mtu yupo busy kuitafuta Euro, siku nina nafasi wenzangu hawana nafasi, kero tupu!(In doors life)
Ubaguzi kwa sana, kama sio mzungu kuna baadhi ya Clubs hata huruhusiwi kuingia. Ukipanda Tram, Trein na Mabasi yao ukienda kukaa seat moja na mzungu ananyanyuka(kukubagua), ama ukitaka kushuka kwenye kituo cha hasa Tram ama Mabasi ya safari fupi, Dereva kama ni mdutch mzungu akikuona ni ngozi mara akupitilize kituo.
Ni kweli, kipato kilikuwa kikubwa sana kulinganisha na ninachopata sasa. Ila ieleweke MONEY IS NOT THE END OF EVERYTING.
Nasema hivi, nina raha sana kurudi Bongo baada ya masomo, pia nashukuru kutoka at least nimewajua kiundani hawa watu na sijutii kuyondoka ulaya (never on earth).
Ulaya hata kama una makaratasi, zaidi ya UK kwa nchi zingine hizi michosho tu, huwezi fanya kazi ya professional yako, you can only do the Dirty job. I am talking through experience kwani nina rafiki zangu waliopo EU wenye paper tayari na kazi zao mzozo, japo wanalipwa vizuri.

Mdau Bongo,


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 10:33:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

its not worth going home, unless, u get a job that promises enough cash even before going back home, so that ukirudi, u know that u have a job that pays equally as u were back in europ. coz companies at home offers really peanuts. lakini ukiamua kuanzisha business yako mwenyewe, nice choice, maybe it would pay. otherwise my advice is, get ur qualifications, find a beutiful gal, marry, get citizenship, work and send money home.
hahah, might sound harsh but its reality.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 10:37:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Ukiwa na Bachelor au Master degree utalipwa Tsh 230000/- (US$2000) kama unapenda kufanya kazi serikali, maana hicho ni kiwango cha kuanzia hakijalishi una Bachelor au Master. Lakini hukiwa huku mamtoni siyo mbaya unaweza kulipwa Euro 1600-2500 kwa kuanzia.
Mzee wa TBS

Tarehe Wednesday, December 5, 2007 10:51:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
Swahili ni zuri sana ndugu muheshimiwa mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba kitu cha kwanza kabisa kwa hapa nje tunapata hela ambayo inakidhi mahitaji yako ya kila siku include bills let say mimi napata £1200 nikifanya na over time yangu naingiza kam £1350,nalipa
rent 200,
council tax 40,
water bill 20,
road tax 15
Insurance 40
fuel 160
gas 20
broadband,tv& tel(package)-110
internationl calling card-20
mobile-20
groceries& toiletries-100 could be more.
my own shopping I cant list I do shop a lot.
misclineous-140
credit card 40+40+20+20
total- 1005
hapo sijajumlisha shopping yangu mwenyewe kabisa ina maana kama sijafanya over time nitabakiwa na £195 in a month sound rubbish to me bora Tanzania unalipwa mshahara wa 1 million or more lakini inatosha or less sijui watu wa nyumbani tupeni statistic zenu na nyie maana wengine tunataka kurudi bongo


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 11:17:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Inaonekana ni jinsi gani mdau wewe usivyo na uhakika wa maisha. SI suala la kujadili kwa sababu mjadala huo waweza kuendelea maisha. Siku zote lipo suali la kiasi gani kampuni gani inamlipa nani kwa kufanya nini ikiwa kapewa hiyo kazi. Dunia hii inazidi kuwa ndogo kila siku. Watu huhama benki moja wakaenda nyingine - miaka ya karibuni nimeshuhudia rafiki zangu wawili mmoja akitoka BOT kwenda CitiBank na mwingine akitoka CitiBank kwenda BOT. Nawajua pia rafiki zangu wengi ambao wengien wameondoka US/Europe kwenda Bongo hali wengine wakiondoka Bongo kwenda US. Hapana formula mdogo wangu - au kama nakuzaa - mwanangu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 11:30:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Kwa nyinyi wenzetu mishio huko ughaibuni hata ishuke bingu hamwezi kuelewa wale tuliosoma na kumaliza tuliorudi tunasherehekea matunda ya uhuru wetu. Huko ni kudanganyana Figure unazoulizia haziwezi kukupa a correct analysis hata kama ukifananisha hizo hela kumbuka gharama za maisha ya huko kwenu na bongo ni tofauti na hapa. Samahani lakini ila ni ukweli kwamba mliowengi huko ughaibuni mnafikiria maisha ya hapa mlipo maana hamna chance ya kufikiria mbele mnabwanwa na shift za kubeba mabox na kunyoa kuku. watu waliorudi huku tunajua raha yake na jinsi maisha yalivyo stress free hapa bongo. There is nothing special we can tell you but "HOME SWEET HOME" hayo mabox mnayobeba huko ni utumwa wa hiari wote tulibeba ila mungu akatupa nguvu sasa hivi tunastarehe bongo ni watu wakubwa tu maofisini. umefikia wakati mkawa werevu mjue kwamba hata usome vipi hawataweza kukupa kazi za maana hata wakikupa uraia huwezi kuwa mwingereza sana sana utakuwa mtanzania mwenye uraia wa uingereza hiyo haiwapi akili?.
Kwa ambao hawajafika ulaya i.e.UK, USA. kama sio raia you can't get a good job utapata zile za kubeba mabox na wazee. WATANZANIA WENZANGU MLIOSOMA RUDINI NYUMBANI KUNA HESHIMA HUKU


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 11:54:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Ni heri wanaosoma digrii wakimaliza wabaki huko huko ili wenye digrii na diploma zilizochoka za Tanzania waendelee kupata ajira.

Vinginevyo wakiamua wote kurudi soko la ajira ni dogo wataumia waliosoma Tanzania.

Kubaki kwao huko nje ya nchi pia ni mchango mzuri wa kusaidia kutengeneza ajira kwa waliobaki Tanzania.Nafasi zao inabidi zijazwe na wengine.

Digrii nyingi za nje siyo Mchezo ni za leoleo na zimesheheni mambo mapya kibao yanayohitajiwa na waajiri ambayo hayapatikani vyuo vya Tanzania.

Wakiamua kurudi nazo wote na kuzileta hapa waajiri wengi watawachukua wao na kuwaacha watoto wa makabwela waliosomea Tanzania.

Walalahoi endeleeni kuomba wasomi wabakie huko huko Nje ya nchi wakishuka hapa kiyama cha kuporwa ajira kitawakuta sababu kisifa ni vigumu kushindanisha Diploma au degree za hapa nchini na za hao walioko nje ya nchi KATIKA MAENEO MENGI TU KIFANI.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 11:59:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

mjadala mzuri binafsi nashauri mrudi bongo kama una elimu kuanzia bachelor kaombe serikalini au government agency ( tcra etc) ,mambo huko ni mazuri walio huko wataniunga mkono , mshahara si mbaya ila marupurupu ni mengi na opportunities ni nyingi,mfano serikalini with bachelor unaanza na tsh 300,000.00 si nyingi ila other benefits ni nyingi na hutashindwa maisha ya kawaida na ya furaha.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 12:06:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Mie sina hio degree ya aina yeyote. Mshahara wangu is over 8 million TS a month kwenye kampuni moja kubwa hapa London. OK i have experience je naweza kulipwa kiasi hiki nyumbani? Napenda kurudi nyumbani lakini kuiba sitaki. Most of Tanzanians(not all) wameiba ili kujenga nyumba zao au kuweza kununua bia. Haya ni maisha kweli? Home is home lakini ukweli kusema kweli mtanisamehe mie nipo huku hadi pension yangu ili nirudi nyumbani kufurahi pesa zangu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 12:15:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

tunapojadili maisha mazuri/bora si sahihi kujadili tu viwango vya pesa.ni vyema tumuangalie binaadam kibaiologia,saikolojia na kijamii.swali hili(iwapo kurudi nyumbani ni uamuzi wa busara au la) halina jibu moja.inategemea na mazingira uliyoyaacha nyumbani na hali yako ya sasa ughaibuni.kwa mfano mtu mwenye ugonjwa ambao matibabu yake yanahitaji huduma ambayo haipatikani nyumbani itamfaa kubaki ughaibuni,mtu anayehitaji kuwa karibu na familia yake iwapo familia hiyo iko nyumbani itamfaa kurudi nyumbani,wale waliona mipango ya kujikita kwenye siasa pia kunawafaa nyumbani.halafu pia ughaibuni ni jina la jumla mno,ni rahisi kwa yule aliye marekani au uingereya kuamua kubaki huko kuliko yule aliye urusi au india kutokana na tofauti za viwango vya kukubalika kwa wahamiaji katika maeneo mbalimbali.tukija kwenye swala la pesa ambalo limeonyesha kuwavutia wengi ukweli ni kwamba katika karne hii jamani tuepukane na mawazo ya mishahara,tufikirie zaidi jinsi tutakavyoweza kutumia mianya ya kuwekeza.Tanzania ina mianya mingi tu katika nyanja ya kilimo kwa mfano.ukijiajiri wewe nwenyewe ndio unaamua kiasi cha pesa unachotaka kutengeneza.watanzania wengi walio ughaibuni wanafanya kazi kweye makampuni binafsi,tutumie hili kama fundisho katika mipando yetu.kisaikolojia,ukishaona unajiuliza kama kurudi nyumbani ni uamuzi wa busara au la ujue kuwa unataka kurudi nyumbani ila unaogopa kukabiliana na changamoto inayoambatana na kurudi nyumbani,weka uoga pembeni.ukiendekeza uoga utakufanya mtumwa.usiogope kuanza chini,iwapo una mikakati madhubuti utafanikiwa.mmiliki wa Dell computers ambaye ni miongoni mwa matajiri wakubwa marekani alianza biashara yake akiwa na dola 1000 tu!na tena aliancha shule ili aanzishe mradi wake(sitoi changamoto kwa wadau kuacha shule,ingawa matajiri wakubwa duniani wana historia ya kuacha shule kama Bill Gates).kila la heri...zemarcopolo.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 12:22:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Maisha ulaya michosho tu, Mimi nimesoma UK Masters, nimerudi zangu Bongoland aah, TAMBARARE you know why?
1. Bongo bwana tunathaminiana wabongo kwa wabongo, nafanya kazi ya professional yangu na kipato ninachopata kinanitosha kwa mahitajai na matumizi ya Bongo, na saving ipo vile vile.

2. Ulaya, kama nilipokuwa UK, sawa nilikuwa naschool lkn ilibidi nifanye kazi kujikidhi kwani sikuwa na sponser na nimetoka familia fukara. Kazi nilizokuwa nafanya mzozo, kusafisha mahospitalini, kubeba box na kuosha vyombo restaurants. Kipato kilikuwa poa kwa kazi zote tatu japo mara unapoteza kazi sometimes, ila sasa nilikuwa CHOKA MBAYA, matumizi juu kodi kibao na rent ndo usiseme, bado nyumbani nitume pesa, sijui simu, in the end naishia kuchoka na sina kitu. Choka hata huo muda wa kutafuta demu wa kunipa makaratasi sina.

Nipo zangu bongoland, ile ndoto yangu ya kuzamia ulaya iliniisha nilipofika huko nikaona hakuna deal. Ninafanya kazi niliyoisomea, malipo yanaridhisha, nipo na familia yangu.

HOME SWEET HOME asikudanganye mtu. Someni mrudi acheni kudanganyana huko, na ndio maana hamuwaambii watu ukweli nini mnafanya, mwaishia kusema mnafanya kazi, hamsemi kazi gani, kuweni wazi.Kudanganyana tu.

Wengine wanaona soo kurudi kwani wale jamaa zao waliwaacha Bongo mambo yao Supper, so wakifikiria inabidi waendelee tu kuwa watumwa ulaya na marekani, kulala wamerundikana kama wanyama kisa mnapishana.

Tena msinikumbushe jamani, nimesuffer UK mimi acheni. Kazi zingine nilizofanya noma hata kuzisema ndugu zangu, Ishaalah, I am back home.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 12:24:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Kama alivyosema mdau hapo juu, dunia ni ndogo sana na hakuna njia moja tu ya kujiendendelezea maisha yako. Si kweli, kurudi nyumbani tu kutanisaidia kujipa heshima na fedha zaidi.
Binafsi, fedha pekee sio muhimu. Kwangu muhimu zaidi ni elimu ya watoto, umeme, maji safi, tiba, na kuishi maisha bila ya kero la rushwa wala na kuwa salama. Nyumbani ni nyumbani na hamu itakuwa rohoni daima kurudi.
Kielimu nina Master's kutoka Marekani, nina uraia wa Kanada pia. Lakini Kanada wanabagua na kwa kuwa uchumi ni mdogo kuliko kazi, wageni wengi wanaoamua kuenda kuishi Kanada kihalali ni wengi sana, inafika watu 200,000 kila mwaka. Kwa kuwa sina mtu alieweza kunisaidia kupata kazi ya maana, nikaamua kuja Japan. Baada ya miaka miwili sasa, nina nyumba yangu mwenyewe, watoto wanasoma elimu ya Kimataifa kwa kulipa dola 100 (Yen 10,000) tu kwa mwezi.(Shule za serikali Japan zinapewa dola 8000 kutumia kwa mwanafunzi kila mwaka na ni bora kuliko za binafsi hapa))

Japokuwa kibiashara niliweza kupata fedha zaidi Tanzania nilipoamua kuishi baada ya elimu ya chuo kikuu, matatizo ya kuishi katika misukosuko ya matatizo ya umeme, maji, elimu nakadhalika yalinikatisha tamaa sana.

Sitaweza kurudi kuishi Tanzania lakini hii ni sababu yangu tu ya kibinafsi, kama alivyosema mdau hapo juu, kila mtu na akili yake na dunia ni ndogo sana, kila raia anasumbuka duniani kote kutafuta riziki, hamna njia moja wala njia ya mkato katika kusaka fedha iwe UERO, TShs au Yen.

Ahsante Ndugu Michuzi kwa kunipa nafasi hapa.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 12:42:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Mwanamuziki Marehemu Marijani Rajabu wa Bendi ya Orch. DSM Int'l alisema 'Pesa ni sabuni ya roho' na 'hata ukiwa mtoto mdogo utapewa shikamoo na waliokuzidi umri'.
Hivyo maisha ni popote iwe ughaibuni ama nyumbani mradi pesa inaingia kwa njia ya kuajiriwa au kwa kufanya biashara halali. Na
utapata 'shikamoo','starehe', 'nyumba nzuri','mke/bibi/mume/bwana mtulivu sababu ya pesa' na pia kama unaendesha biashara zako mwenyewe pia utawaajiri watu na kuwalipa mishahara mizuri tu na kuendelea kuwa maarufu na kuheshimiwa popote ulipo ulimwenguni. Hivyo swala siyo urudi nyumbani au ubaki ughaibuni suala ni jinsi ya kutengeneza PESA kwa njia ya halali popote utapo amua kuishi ulimwenguni iwe Alaska,Uruguay,Tanzania, Vanuatu au Montenegro .
Nawashilisha Hoja.
SeniorJunior
London.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 1:10:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Kwa wale wanaoamini kuwa Mungu ndiye katuumba na hatujatokana na mambo ya evolution watakubaliana na mimi kuwa kweli tumeumbwa kwa mawazo na akili tofauti.

Hapa mimi sioni cha kujadili kabisa, maana mjadala utakuwa mrefu sana na wala hatuwezi kufikia suluhisho.

Ushauri wangu ni kuwa, kama mtu kweli unawapenda wazazi/walezi, jamii yako au ndugu zako uliokua nao tangu utotoni na ukafikia hatua ya kupata fursa ya kwenda kusoma nchi za ng'ambo, ujue fika kuwa hivyo vitu ulivyovikuta huko (usafiri mzuri, maji ya moto na baridi, makazi yanayoeleweka, nk)ni hao uliowakuta huko (wenyeji) ndio walisota kuviweka in place, kwa hiyo usidhani hata siku moja kuwa wanafurahia wewe ku-share nao hivyo vitu. Rudini nyumbani mlijenge taifa ili kama unakuona kwenu ni kubaya na wala hakulipi, uje upatengeneze ili pawe pazuri na si kupakimbia!

Mtanzania Mweusi


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 1:23:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Jamani jamaa anataka uzoefu ili imsaidie kufanya maamuzi, najua kama uliishi mahali muda mrefu inakuwa ngumu kufanya decision kwa sababu ya fear ya usichokijua ni ubinadamu kuwa na hofu ya usichokijua.

Labda mimi kwa uzoefu wangu tu, mimi nilisoma degree ya kwanza na ya pili huko huko Bongo na nikapata kazi kwenye kampuni binafsi ya nje. Mshahara wangu ulitosheleza mahitaji yangu ya kila siku na kujiwekea akiba. Huna haja ya kujua figure/kiasi kwa sababu itakuchanganya maisha ya Bongo ni rahisi sana huwezi linganisha na huku. Halafu nikahama Kampuni nikaenda kwenye NGO ya Nje ambayo inashughulika na uhifadhi, huko nilikuwa nalipwa kwa US $ kwa mwezi mbali na allowance nikiwa porini. UPo hapo, napo nikaacha kwa sababu za kifamilia (mie ni mama mwenye watoto, uzazi ukanifanya niache kazi za porini) Nikarudi tena kampuni nyingine binafsi ambako nilifanya kazi mpaka hapo nilipoacha kwa ajili ya kuja masomono huku Ukerewe kwa degree ya tatu. Na nikimaliza narudi zangu Bongo, nimeshajua hali halisi ya huku hanidanganyi mtu na hali ya Bongo nilivyoiacha najua nikirudi nitapeta.

Kwanini nasema nitapeta? Wengi wanafikiria kuhusu kuajiriwa, mie hilo nimeliweka kama namba mbili shughuli zangu zikigoma, nataka kufanya shughuli zangu mwenyewe Bongo kuna opportunities kibao mradi tu mtu uwe mvumilivu na ufungue macho kuona opportunities zinazokuzunguka. Nataka kutoa mfano mdogo tu ambao wengine wataudharau na kuona ni wa kipuuzi kuna jamaa ana shamba la kufuga kuku wa kisasa, ame invest huko kwa mwaka anaingiza milioni kama 80 kabla hujatoa gharama. Na hizo ndizo anazotamka hatujui anapata kiasi gani tena hiyo ilikuwa wakati bei ya kuku iko chini, wakati ilivyopanda sijui alikuwa anapata kiasi gani ndiyo kazi yake hiyo pamoja na kisomo chake. Kuna mwingine na degree zake yeye ameamua anakodi mashamba na kulima nafaka, kilimo cha msomi si mnakijua, basi mambo yake nayo ni supa.

Hapa nilitaka kuonyesha tu shughuli za kufanya zipo sio mpaka usubiri kuajiriwa, mie shughuli ndogo ndogo nilitaka kujaribu lakini kwenye private company watakulipa vizuri na huwezi kupata nafasi ya kufanya hizo shughuli waliopo serikalini wengi wanafanya shughuli nyingine pembeni kwa sababu wanapata muda huwezi kumwambia jumamosi na jumapili aje ofisini huyoo shambani kwake kwenye kuku, ngo'mbe wa maziwa na shughuli nyingine ambazo zinawaingizia kipato cha ziada cha kuweza kusomesha watoto wao.

Huku wenye kutaka kubaki abaki lakini ni kuzuri tu kwa kutafuta elimu na kwenda mahala ambako elimu yake itatumika ipasavyo huko Africa, sio lazima urudi Tanzania, ukisikia kazi imetangazwa na mashirika makubwa kokote Africa kama unajimudu apply, ninao marafiki ambao wanafanya kazi Southern Africa kwenye University na sehemu mbali mbali kama West Africa kama lugha zaidi ya moja inapanda (French, Arabic).

Maisha ni popote bora utu na heshima yako vithaminiwe.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 1:29:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Msomi ambaye hataki kurudi sababu anasema nchi inalipa malipo madogo ni mvivu na mjinga na anayetakiwa asome zaidi siyo ulaya au marekani bali arudishwe Afrika au abaki huko huko asirudi Tanzania.

Ni lazima wasomi wajue kuwa huko wanakolipa vizuri watu walifanya kazi kwa juhudi na maarifa kwenye chumi zao na makampuni yao mpaka yakafikia huo uwezo huo mkubwa wa kumlipa hata mbeba box pesa nyingi kuliko waziri aliyeko Tanzania.Hawakuwa wavivu kuanzia kufikiri hadi kufanya kazi

Swali je ni nani anatakiwa atengeneze makampuni mazuri yatakayolipa vizuri kwa ajili ya Watanzania wanaorudi toka nje ya nchi? Je ni hawa maskini wenye elimu duni mliowaacha kule Tanzania waliosoma chini ya miembe shule za msingi zisizo na madawati ndio mnataka watengeneze hayo mazingira na wasomi turudi kama wafalme kula kuku kwenye hayo makampuni ya walalahoi?

Aibu wasomi aibu tufike mahali tuone haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

koloboi@yahoo.com


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 1:33:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

I confess home sweat home, nakufanya kazi nyumbani raha sana, na kunaheshima kubwa, na maisha hayatizamwi katika kipimo chapesa peke yake kuna vitu vingi vinavyoyafanya maisha yawe mazuri ukiachilia mbali pesa,ninachopenda kusema kwa wasomi walioko ulaya kuwa na foundation ktk maisha ni jambo muhimu sana na huko ulaya ni sehem nzuri ya kupata hiyo foundation in term of basic needs, ukiwa unafikiria suala la kutafuta kazi huko bongo, kama mtu si chapombe kupita kiasi na starehe za kijinga wakati wa kipindi chake cha masomo anaweza kusoma na kubeba box , akarudi napesa nzuri ambayo itamsaidia ktk kuweka foundation ya maisha yake huku akisubiria kazi, so ushauri kwa wale ambao wameamaliza na hawana foundation za maisha wanaweza kubeba box kidogo then warudi ila wasiiishi moja kwa moja, utamu wa maisha upo home.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 2:03:00 PM EAT, Mtoa Maoni: mpare masai

Kilichonifurahisha ni kuwa kuna watu wamekuwa wakweli mtu ameeleza hajui kilichopo mbele yake anaomba msaada. This is very good. mpeni msaada kwa wale wenye experience wengine na form four yetu mkizungumzia bachelor au masters, mnatuacha, but that's a challenge, man i like it.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 2:31:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

nionavyo mie, kaa ulaya ila husisome zaidi ya shahada ya kwanza sababu hutaitumia elimu yako ipasavyo au soma, urudi nyumbani ujenge nchi yako. naamini hata wao kuna ambao walisota miaka ya nyuma na ndio maana sasa wanamudu baadhi ya vitu. bora nipate mshahara mdogo lakini roho haisononeki kwa kuamrishwa na watoto wadogo kisa wazungu. mgeni hathaminiwi! mungu nisaidie, vyeti vitimie nirudi nyumbani, nikajenge nchi yangu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 2:35:00 PM EAT, Mtoa Maoni: kb

nyumbani ni nyumbani!
lazima uone tofauti ya kiuchumi iliyopo kati ya huko ulipo(usa&europe)hivyo uwezi compare salary au kutaka ukija bongo ulipwe kwa kiwango cha huko nchi zilizoendelea labda uje kuajiriwa kwenye international organisation.

serikalini mshahara wa graduate ni TGS D hii inacheza kati ya Tshs.150,000/= mpaka 230,000/=ni kwakuwa unaweza pata safari,lunch na overtime,kidogo maisha yana kwenda.

kwenye private sector au mashirika yanajiendesha vizuri na kulipa wafanyakazi wake vizuri nayo mshahara wa graduate wa kuanzia ni Tshs.400,000/= mpaka 1,500,000/=(haya ni mabank,kampuni za simu za mikononi,NGO's,hospitals etc)

life style ya bongo kwa kipato cha kuanzia tshs.1000,000/= unaweza kuishi maisha mazuri tu.

kwahiyo acha woga na ofu maliza shule rudi nyumbani najua utakuwa ushatatua matatizo kama ya usafiri(gari,nyumba/pesa yake) na vitu vidogo vidogo ambavyo kwa bongo ni bei juu,hapo utaishi maisha standard.
but please dont compare everything with europe uatakuwa frustrated hizi nchi zetu ni still very poor!

maisha ya graduate kuishi kwa kubeba box,kuosha vyombo,bar man/maid,cleaner,kuosha wazee,utakuwa frustrated mapema sana ingwa unapata a lot of money.and you will end up semi professional1


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 2:42:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Kada

Sikiliza fedha sio mafanikio. Na wala hazitakupa faraja hapa Duniani bila kupata maisha unayoyataka. Amsha akili fanya KILE UNACHOTAKA KUFANYA. Mimi sio msomi kama wewe lakini ninamaisha kuliko wanaojiita wasomi. Walioko ulaya na hata Tanzania. Nimeridhika na mpango wangu wa maisha. Narudi kwenye agenda yako unaweza kufanyakazi nyumbani ukapata mshahara mdogo lakini ukawa na kazi ile unayotaka kufanya na ukafurahi kwa maisha uliyanayo. Na unaweza kubakia huko uliko ukapata kazi uliyosomea ukaishia kunywa na kupata mashinikizo ya damu. Kwakweli hakuna mtu atakaye kupa jibu sahihi hapa. Sikiliza mawazo ya watu amua tuu uamuzi wako UKIFANYA KILIE AMBACHO NAFSI YAKO YA NDANI INATAKA UTAFANIKIWA POPOTE PALE DUNIANI. Siamini kama Pesa ni swala la kuzungumzia hapa. Mimi napata mshara 25000 DANISH KRONER baada ya Tax zinazo ingia mkononi mwangu yaani 15000 ambayo ni 3,150,000Tzsh Nyumba nalipa 6000dkr ambayo ni 1,260,000 ukichangaya na mahesabu mengine ghahama tupu. Kumbuka familia zetu ukiwa nje. Sio lazima uwatumie lakini lazima utawatumia. HIVYO MWANA GLOBU HESHIMU MAWAZO YAKO NA MIPANGO YAKO. Nadharia yangu inasema hivi usichezee mpaka wa nchi. Maana ukivuka mpaka wa nchi maana yake vitu viwili.Pesa au Elimu. Kimoja kati ya hivyo lazima urudi nacho nyumbani. Na sio matusi wala makelele. Natumaini Mathupu ataipitisha hii ili angalau uisome. NB: NILIKUA NARAFIKI AMBAYE ALIKUA MSOMI WA JUU SANA ALIAMUA KURUDI KWAO. KWASABABU ALIPEWA KAZI LAKINI MASAA YAKE YALIKUWA MACHECHE SANA. MAISHA YAKE YALIKUA MAZURI LAKINI ALIJIKUTA ANATUMIKA. HAO WANAOKUAJILI SIWANAJUA KIWANGO GANI HUKO KWENU WATU WANAPATA?. HIVYO UJUE KUTUMIANA KUPO TUU. NAKUTAKIA KILA LA KHERI ILA NAKUOMBA SANA HESHIMU MAWAZO YAKO NA MATAKO YAKO.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 2:58:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Ndio maana ndugu yetu kauliza!!
Mdogo wangu mambo ya bongo hayana formula!!kama jina lenyewe bongo! Kwa kuanzia ""where your heart is?"" hilo ni swali la kuanzia, mbili vipi unapasua kiasi gani?
tatu,course unayo soma!
Tupo hapa(tumerudi!!) na wasomi kibao, wengine walikuwa ni siku zote ""A""! si wengine wa average!! sote tumeanzia chini na sasa tunasusua na 2,000,000.00tsh na wengine inshallah wapo juu sio mchezo! na mapambano yanaendelea! wengine wamerudi huko majuu, kuna nchi kama Dubai, Canada, south Africa wote hawa wamerudishwa huko baada ya kupasua mambo hapa hapa bongo hasa baada ya kuchoshwa na sinema za Bongo!!
Kwa hiyo mdogo wangu usitishike kurudi ""where your heart is"" is first to think! Karibu tuongeze nguvu!

Mzee wa Mwanza.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:00:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Mimi nimesoma undergraduate hapa hapa bongo, na Masters yangu hapa hapa. Najilinganisha na wenzangu wenye elimu kama yangu huko ughaibuni ninapokuja huko mara chache kwenye vi semina nawaona wako hoi, hawana raha. Wako busy, wanaishi na wasiwasi kwamba wabaki huko au warudi Bongo. Na wale wanaorudi huku Bongo utawaona walivyochoka, ila baada ya muda wanaanza kutakata. Ndio sababu sasa hivi ni nadra sana kukuta kinana yuko bongo kapata kazi yake, ana take home ya $1200 afikirie kuja huko muliko. Gharama za maisha hapa ziko chini, muda wa kupumzika upo, kwa ujumla maisha ni mazuri. Infrastructure zinaboreshwa kila siku. Na ni rahisi kutengeneza future ukiwa hapa. Ila tunawashukuru mulioko huko kwamba hicho munachokipata, kinarudi nyumbani (Western Union foleni sio mchezo). Ndugu yangu usiogope kurudi nyumbani, pako bomba tu.

Mzawa - Masasi


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:11:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Dr. Confusion

Very nice and brilliant question!Mimi nadhani hapa inategemea perceptiveness ya mtu,kuna viumbe vilivyojijengea akilini mwao kwamba kuishi nje ni kuukata kutokanana na ukweli wa kwamba baadhi ya nchi zilizoendelea hakuna malaria,hakuna kipindupindu wala magonjwa yanatyochangiwa na “umasikini”Vilevile kuna wale basi tu wamekwishachukia mfumo wa maisha waliokuwa nao baada ya kipofu kuona mwezi basi tena ndo nyumbani kubaya.Ni ukweli usiopingika maisha ya nyumbani yamegawanyika sana kuna wenye kipato cha juu na wanaotesa na kunawengine ndio wanateseka

Mtazamo wangu ni kwamba masisha ni pale mtu amabapo unaweza kukidhi haja zako na ndoto zako,kama unaona ni vyema kuwa na vyeti vikubwa na kutumikishwa kwenye kuosha vyoo,beba box,tawaza vizee,endesha malori ,kukosa uhuru na kutengwa na kubaguliwa katika sehemu za kazi,it is fine.Magezeti ya hapa Uingereza sasa hivi yamesheheni habari ya yule Mwalimu aliyetuhumiwa Sudan,lakini baadhi ya magazeti hayaongeleeni Sudan kama sudan yanazungumzia Africa,it is because that is the way of persciving issues.

Maisha ya nyumbani ni mazuri sana kwani hata wakati mwingine hujifananisha na ile hadithi ya mimi najifia na kuteseka porini wakati SADIKI ashiba nyumbani kwa baba,ingawaje hakuna usalama,majambazi kibao,uhuru kamili hakuna,mishahara inategemeana na wakubwa ndio wenye maamuzi.

Shime tuache dharau ya kutukana nyumbani wakati huku twatukanika na Monkey business,kama hayajakufika basi yatakuja kukusibu tu!Nyumbani pia tende na mabadiliko ya kiuchumi,mikataba ya ajabuajabu,na mikakati ya kufaidisha wachache itokomezwe kabisa.
Dr Confusion aka Mzee wa kuchanganyikiwa na kuchanganya


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:12:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Mie na mke wangu tunakusanya $160,000 baada ya tax, mwajiri gani nyumbani atakuwa tayari kutulipa hata nusu ya mshahara huo!? Umeme wa uhakika, Maji belele hata wasi wasi wa kukosa maji au umeme kwa miezi chungu nzima hakuna. Barabara nzuri na ajali ni chache mno. Sina haja ya kutoa au kupokea rushwa ili kuishi maisha mazuri au kupata huduma muhimu toka popote pale. Sasa mnatuambia turudi nyumbani eti kuna heshima!? Heshima gani iliyukuwepo ikiwa unatakiwa utoe rushwa ili kupata haki yako? Acheni mawazo finyu siyo kila Mtanzania aliye UK, US, Canada na kokote kule wanaosha vyombo au kubeba maboksi asilimia kubwa wana kazi nzuri sana na wanapata hela safi sana lakini hawana ngebe.

Wengi hatuna mpango wa kurudi Bongo kesho wala keshokutwa. Nyinyi endeleeni na kuuza nchi kwa wageni.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:15:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Hii mada nimeipenda sana!!, mimi ni mtanzania nina kama miezi 3 toka niingie Austria kwa masomo (masters), nyumbani nafanya kazi serikalini silipwi mshahara mkubwa ni chini ya laki 3 kwa mwezi.Lakini toka nifike hapa sijaona uzuri wowote wa Europe kama watu wengi wanavyofikiria hasa ambao hawajawahi kufika huku.Ndio unafanya kazi unalipwa mshahara mkubwa lakini gharama za maisha nazo zipo juu, unakuta mshahara wote unaishia kulipia nyumba, mafuta ya gari, umeme nk!Ni bora bongo unapata kamshahara kako kadogo ila kanakutosha kwa mwezi kufanya anasa zote unazopenda na bado unabaki na balance!!, Ukweli ni kwamba wa afrika wengi waliopo hapa nilipo hawana kazi za maana, zaidi wanasambaza magazeti usiku na wengine wanasafisha vyombo na kufanya usafi migahawani. Ukweli ni kwamba sitamani katu kubaki huku baada ya kumaliza kusoma, ni bora nirudi zangu TZ niishi kwa raha na mshahara wangu mdogo. Jamani kama una nondo rudi nyumbani. Kama unabaki Eu hakikisha unafanya kazi uliyosomea na sio kubeba Zeboxes!! Kwa ninavyoona mimi hii miezi michache niliyokaa hapa Austria naona nyumbani maisha mdebwedo tofauti na Eu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:28:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Unajua vijana wa kitanzania sijui ndiyo ulimbukeni au kusoma na kutoelemika ndiyo tatizo linalowasumbua, au ndiyo ule usemi usemayo hiari yashinda utumwa? Hivi bado hamjagudua tu kuwa hapo mpo kama watumwa wa hiari? Chonde chonde jamani rudini nyumbani na maisha ya huku siyo kama mnavyofikiri ila labda mnaogopa kurudi kwa sababu hata shule mliyoendea hamjasoma mmebaki kubeba maboksi? Mi ninachojua wengi ambao kweli wamefaulu vizuri huko ulaya wamerudi nyumbani na matunda wanayaona na mliobaki ulaya najua utumwa wa hiari ndicho kitu kinachowasumbua na uoga kuona kuwa wale mliowatambia kuwa mumeukata wako mbele kimaisha kuliko nyie.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:41:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Sasa nasema hivi kama haujarudi bongo toka umeenda huko bora rudi uone mabadiliko yaliopo kwa sasa.

sama


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 3:56:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Where the happiness and satisfaction concide that is the place to stay,a place to live. Mengine yoote yapo maana kero na raha vipo dunia hiihii iwe ulaya,au africa. Dunia ina pande nne si kila mmoja wetu atafanikiwa akienda East,pengine akienda North atafanikiwa,labda West au South,labda pengine akiwa centre.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 4:07:00 PM EAT, Mtoa Maoni: constantin

huu mjadala ni mzuri sana, hapa kuna mambo kadhaa ya kuangalia, kwanza kuna wabongo wengi tu wapo ulaya na marekani lakini hawasomi bali wanafanya hizo kazi za hovyo (les boolots sales) in french or dirty jobs in english. kwa hiyo hawana ujanja wa kurudi bongo kwani hawataweza kuhimili ushindani katika soko la ajira. pili naungana na mmoja wa watoa maoni hapo juu kuwa pesa unazopata ukiwa ulaya zinaonekana nyingi sana in terms of figure mfano euro 1600 ni kama milioni 2 za tz ambazo ni zaidi ya salary ya mawaziri na wabunge lakini kwa hapa ulaya sio kitu kabisa, inakufanya u survive tu, hebu angalia kuna maelfu ya wahaiti, wa nigeria na wajamaica huku ulaya lakini bado katika nchi za kuna kiwango cha juu mno cha umaskini ina maana vipato vyao vinaishia kwenye kukidhi mahitaji yao hapo ulaya.
suala la tatu ni ulimbekeni wa baadhi ya watu ambao wanaona ulaya kama peponi ambao hawajui kuwa bongo ukiwa na pesa kiasi unaishi kwa starehe mara mia ya ulaya, hivi tujiulize utabeba box hadi lini kwani ukiwa mweusi hawawezi kukupa kazi ya ofisini hata siku moja. suala la nne ni kutojua kuwa pesa haiwezi nunua furaha hebu angalia nchi kama finland moja ya nchi tajiri kabisa ulaya, imeizidi kwa mbali nchi ya wabeba mabox lakini ina kiwango cha juu cha suicide, hii inaonyesha wazi pesa inavyoshindwa kumpa mtu furaha ya maisha.
na mwisho, kama umebahatika kupata elimu bora huko ulaya, unaweza kupoteza ujuzi wako kama utaendelea kubeba box,napenda kuwapa moyo kuwa bongo bado kuna oppurtunities nyingi sana, na mtu akitumia exposure aliyoipata ulaya anaweza kupiga hatua kubwa sana bongo, mtu anayepata sh.laki 7 bongo ana standard nzuri ya maisha kumshinda mtu anayepata pounds 1300 huko uk.
jamani nyumbani ni nyumbani cha msingi ni kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kurudi, hofu yangu kubwa ni kuwa kadiri umoja wa ulaya unavyopanuka, kutakuwa hakuna hitaji tena la watu weusi,kwani kuna baadhi ya nchi ukienda kazi zote za hovyo zinafanywa na wazungu maskini kutoka ulaya mashariki, mnaoishi ulaya mnanielewa katika hili, wenye akili zao hukaa ulaya na marekani kwa malengo then hurudi nyumbani na sio kuzamia


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 4:11:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Wadau wote hapo juu mlioongea mimi nawaunga mkono. Lakini pia kwa mawazo yangu mimi nafikiri kupata kazi ughaibuni au Bongo yote ni bahati. Mimi binafsi, kwa sasa nipo Ubegiji nilikuja kusoma Master degree hapa, na baada ya kuhitimu department ambayo nilikuwa nasomea wakanipa kazi ya mkataba wa miaka mitatu, na inalipa kulingana na viwango vya serikali ya Ubelgiji kama supporting staff sio Lecturer (Kwa kuwa sifanyi kazi ya U-Lecturer), ila nafanya kazi kwenye center kama Data analysis officer na ninalipwa Euro 2,720 kwa mwezi, na naona wenzagu ambao ni wazungu tunalipwa sawa na wengine nawazidi tena mimi naonekana mtaalamu wa bara la Africa.

Hivyo mimi nafikiri is just the matter of opportunity, kama mkataba ukiisha basi narudi home, siwezi kujibana huku kwa kufanya kazi za ajabu ajabu.

Mdau wa Ubelgiji.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 4:13:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Jamani ndugu zangu mimi nimewasoma wote tena vizuri na kwa ufasaha. Hapa tuna mambo 2 ya msingi lazima tuyaelewe. Moja Kuna suala la Serikali kujipanga ili kuweza kutosheleza mahitaji ya wananchi hasa wasomi na wengie kwa ujumla kwa maana kupunguza ubabaisha,urasimu,ukabila,kujuana na utoaji wa huduma bila kuiweka mbele rushwa kwa wananchi hasa wasomi wa Kitanzania ndani ya nchi yao. Pili kwa wananchi sasa hasa wasomi watambue kwamba nchi kama nchi kukua kuichumi na maendeleo kunatokana na mchango mkubwa wa wananchi wenyewe. Sikatai watu kwenda kusoma na kufanya kazi nje ila lazima uangalie hadhi na heshima ya kazi unayoipata huku uliko licha ya kwamba unapata pesa nzuri ila ndani ya roho kunakusuta. Kwa ujumla wake naamini kwamba nje kweli kuna lipa ila mazingira sio yenye UTU sasa basi kwa kujumuisha uboreshaji na mipango ya nchi, serikali inabidi ijipange upya kuhusiana na ajira hasa kuzingatia kiwango cha elimu ya mtu binafsi na Mshahara wa kujikimu kulingana na maisha yanavyokwenda. Naamini kama kutakuwa na maboresho sidhani kama wasomi wetu watang'ang'ania kubaki kwenye Kuchambisha vibibi na kubeba Box.

Tanzania inawezekana ila kinachoharibu ni wale walioaminika katika ngazi za juu kutokujali maisha ya watu wa kati na wachini.

Ughaibuni kuzuri kipesa ila sio kama Nyumbani kiutu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 4:31:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Cha chandu

OOOhhh this is now s***&$$%% and crap!!!kwa sababu kila leo watu wanajadili upupu WHY?WEnzenu toka China,Japan,Asia yote kila siku wanakazana kujazwa kwenye makontena destination UK nyie mnajadili kipi ni kipi.
Just in short apply "MASLOW'S Hierarch of needs". Someone want to be Prime minister,another one to drive Toyota Balloon but living in no water or no electricity house,another one, just want safety and Physiology(basic) needs.
Hapo tuu mmepata majibu yote.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 4:46:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Tim

Habari bwana Michuzi............

suala la mshahara haliaangalii umesoma ulaya wala marekani, lahasha.bali ni experience na deriverience yako katika kazi utakayofanya.......hizi fikra za kwamba watu walio nje ya nchi wanalipwa vizuri ni mbovu......pesa unayopata nje ya nchi ni ya kukuwezesha kuishi kule lakini si kuweza kuendelea, matokeo yake wanapoludi hapa Nyumbani wanaadhilika kwa kuwa wanakua wamepoteza muda wao mwingi ulaya wakati wenzao walioludi nyumbani wana prosper (matawi ya juu) people come back home TULIJENGE TAIFA.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 5:29:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Abraham Harold Maslow Mwenyewe

Umsome vizuri huyo Abraham Harold Maslow na hizo "hierarch of needs" zake!

Ni ubinafsi, "per excellence!"

Ubinafsi, ubinafsi, ubinafsi ni chanzo cha matabaka na "apartheid-form" ya mipango ya maendeleo!!!

Prof. Issa Shivji, uko wapi? Naona baadhi ya hawa vijana "are not getting it (the message)!"

Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, Abraham Maslow, kwani kakwandikia wewe m-Matumbi au kazi yetu sisi ni kula hata yale tunayoyaona kuwa ni "marapishi"?

Someni. Eleweni. Na mjaribu ku-"externalize applications" ya yale msomayo!


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 5:36:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

We annon Wednesday, December 5, 2007 3:12:00 PM EAT unaonekana jinsi gani ulivyo mshamba mkubwa na mwongo. Kama unapata US 160,000 kwa mwezi baada ya taxi unafanya nini huko Majuu MUDA WOTE HUU?!
mimi nadhani ungepanda ndege uje uinvest bongo na kusaidia kuondoa hiyo unayoihita RUSHWA. Hakuna sehemu duniani hakuna rushwa. lakini kila moja inakuwa defined na mazingira. Sasa wewe kupata mshahara huo wa USD 160,000 kwa mwezi na baba yako huku Tanzania akiwa anapata USD 230 kwa mwezi huoni kwamba tayari hiyo ni rushwa ya kiakili?!! Rudi nyumbani acha ulimbukeni. Unadhania hizo barabara zilijengwa na shetani na maji bwelele yalimwagika kutoka mbinguni!

Yaani Wabongo kweli kazi sana!. Ije ifikie time angalau tuweze kufikiria kama wa-SA itasaidia sana.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 5:44:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

wala mavumbi mnachemka,sie kurudi huko ni maajaliwa ili mradi familia huko wanaishi uzuri poa.ila kurudi tena huko macho yazidi kuwa mekundu noooo.Nimeshafika hapa pepa zimekaa pouwa,yes niache nifaidi matunda yangu au vipi.unirudishe nikakutane na "nguvu mpya,kasi mpya na ari mpya"kumbe ni changa la macho,NNNNNOOOOOOO,mavumbini sirudi.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 5:49:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Naelewa watu wanaposema nyumbani ni kuzuri na maisha bado poa. Lakini nauliza hiyo nyumbani kwa nini inakuwa ni mijini tu.Ukiangalia wote wanozungumzia kuhusu nyumbani hamna hata mmoja anayezungumzia maisha nje mji.Watanzania wengi tumetoka vijijini lakini kimbilio letu kubwa limekuwa mijini kwa sababu tunaamini mijini ndio kwenye maisha bora.Na hii ya sasa watu kuanza kutoka nje ni wigo mijini kumejaa.Watu tulioko nje wengi tunaamini sasa hivi nyumbani matatizo ni mengi hawa wote wanaosema maisha ni tambarare ni wachache sana, lakini watu wengi maisha ni mchapo.Ni wachache wanafaidi matunda ya uhuru.Asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi kwenye umaskini.Sasa jamani wengine tunaona ni bora kuishi kwenye umaskini huku nje kuliko umaskini nyumbani


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 6:04:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Nilipokuwa Tanzania miaka mitano iliyopita mimi na mke wangu wote wasomi, tulikuwa na mishahara kwenye milioni chache hivi. Poa kabisa. Baada ya kutua Ughaibuni, tulitulia, na tukaamua kula elimu zaidi tena. Hivi ninavyozungumza kufikia mwakani (wote tukiwa hatujafika hata umri wa miaka 40), wakati kama huu tutakuwa tunalipwa wastani wa dola 250,000 kwa mwaka mbali ya marupurupu mengine na huduma. Unafikiri miaka mitano kutoka mwakani tutakuwa tunalipwa ngapi? Tulifanikiwa nyumbani na sasa tunafanikiwa huku, hivyo maamuzi yetu yanategemea vitu vingine kama vilivyotajwa hapo na waliotangulia, sina haja ya kurudia. Si kila mtu aliyeko huku anabeba boksi. Na tusidanganyane, miaka karibu 50 tangu uhuru nchi yetu haijafika popote wakati Korea Kusini, Singapore, Malaysia, na zingine zimetumia muda huo huo kufika mbali mno. Sisi hatuna ubavu kama huu kutoka na asili yetu na tabia tulizojijengea tayari. Kusema eti tukirudi tutabadili mambo ni kujidanganya. Wanasiasa wanaiba, wanauza nchi, wazungu wanajichotea madini kama watakavyo, Makaburu wanachota, Wakenya wanavamia kila kona, ni Watanzania wachache sana ndiyo wanafaidika na mabadiliko haya hasi yaliyopo sasa nyumbani. Nitapajenga Tanzania kutokea huku siyo kwa kutoa kafara maendeleo ya familia yangu. Sidhani kama miaka kumi kutoka sasa sehemu kubwa ya wanaodai eti wanafaidika na kufanya kazi Tanzania watakuwa wamefikia hata nusu yangu kama hawatakuwa mafisadi na wala rushwa. Haya mambo yanategemea vitu vingi, kila mtu ana nafasi yake peke yake na kipimo chake. Mimi leo hii sina shule ya mwanangu kusoma Tanzania yenye ubora wa iliyopo hapa nilipo. Tanzania unaweza kufa kwa kukosa huduma nzuri ya afya hata kama una fedha, kisa eti vifaa duni na madaktari wavhovu. Huku sina wasiwasi. Kuna mambo mengi ya kuangalia washikaji siyo kuropoka tu na kujitosa.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 6:05:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Jamani dunia ya siku izi imekuwa kama kijiji tu. Kazi ni kazi na waweza kuifanyia mahali popote pale ila mradi unarizika na unachokifanya iwe tz au usa. zamani ulikuw auktoka musoma kwenda kjufanya kazi Dar unaonekana kama umekimbia kuchunga ng'ombe na kwamba hutaki kuendeleza Musoma, siku izi ukienda ulaya unaonekana pia umekimbia shinda za tz.

Dunia ya leo ni kuangaika tu, si mnawaona wazungu nao wanakuja afrika kutafuta maisha? wacheni na vijana wetu waenende huko kwa wazungu wakatafute maisha.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 6:20:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Mtanzania Halisi

Haina maana kusoma UK na kulipa zaidi ya milioni 15 za Kitanzania halafu ukaishia kuosha vyombo, kusaida wazee, kufanya usafi wa mahoteli na sehemu nyingine, wakati ukienda Bongo kwa elimu yako unahakika ya kupata kazi na kufanya kazi ya kile ulichokisomea. Kama lengo nikuishi hapa na kufanya kazi zao za kishenzi, basi ni bora ukaishia kufanya vidiploma vya afya na vinginevyo ambavyo vitakusaidia ili uweze kuwa mtumwa mzuri.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 6:30:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Wandugu,Unajuwa ukizungumzia maisha bora, uelewe unagusa individual life. HApo kila mtu atasema kadiri anavyojiona ama anavyoishi. Hata hii leo ukiwailiza wabongo walio hukohuko bongo wanajisikiaje kimaisha wapo watakao kwambia magumu japokuwa wanalipwa mishahara mikubwa kama mnavyojisifia. Zipo nchi za nje zenye upungufu wa wataalamu mfano Canada hadi hii leo inaingiza wataalamu kibao kutka nje kuja kufanya kazi huku wakiwemo wabongo wenye utaalamu mkubwa na ninafikiri ndio wenye mishahara mikubwa huko. Ni vigumu kwa mtu mwenye status ya hapa kushawishika kurudi bongo eti atapata kazi nzuri. Canada wengi wetu tuna status na ikiwa huna una nafasi ya kuipata labda uwe mvivu wa kuiwinda. Hapa ukilamba masters tu tayari ushapenya na mwaka sasa Mungu akupe nini? Jamani kurudi bongo ni wajibu wetu ila tuangalie ukweli je, zile ajira milioni kumi za JK zimeshasaidia wangapi? Kwa nini tusiishi huku kwenye ajira mara mbili ya hiyo ahadi ya JK? SI WOTE TUISHIO NJE TUNABEBA MABOX.Tupo wenye kazi za maana na pengine hazipo huko bongo mfano fani ya subcomputer communication ipo wapi bongo? Fahamuni wapo wabongo huku tukirudi huko hatuna ajira kutokana na ukweli tunaelimu ambayo bado haija exist huko mliko. UKWELI NI KWAMBA NJE NA FANI YA BIASHARA NA MANAGEMENT BONGO HUNA KAZI YA MAANA WALA USIRUDI. AU UKUBALI KUUWA FANI YAKO. MAANA HATA HIYO SAYANSI SI ILE ULIYOISOMA CHUONI HIVI KARIBUNIUKIWA HUKU.

Mdau toka Canada na sasa ni mkenediani kama inavyotamkwa na wenyewe ambao ni sisi.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 7:08:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Nakubaliana na hapo juu, dunia tunayoelekea distance itakuwa siyo issue kabisa. Ngoja nikupe mfano: Mimi niko hapa U.S.A muda mrefu, lakini nakwenda kutembelea wazazi kule kijijini Tanzania mara nyingi kuliko ndgugu zangu waliopo Dar, kisa: I can afford it more, vivyo hivyo communications, mara nyingi nitapiga simu kijijini na kuwajulia hali mara nyingi zaidi ya ndugu zangu walio Tanzania. At the same time, nikiondoka hapa kwenda nyumbani nafika huko haraka au mapema zaidi kuliko wale waliotoka Dar at the same time kwa mabasi. Na wakati huo huo, nina kazi kwenye profession yangu, na ninashindana na Wazungu na wengine nawazidi malipo. Sasa ungekuwa unanishauri ungesema kweli nirudi home just like that? Halafu nawasaidia ndigu zangu kwa ukubwa sana tu. I love my people and my county so much, lakini naona kwa sasa hivi hapa panalipa zaidi kwangu binafsi na familia yangu na ndugu.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 7:42:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Dar.millionaire

Jamani hatuwezi kuwa sawa. Kikubwa ni kila mtu atathmini maisha yake na aamue wapi panamfaa kuishi at the moment.

Kikubwa ni tushirikiane kujenga nchi. Tujenge mahusiano ya kibiashara kama watanzania regardless tuko wapi. Na washamba kama kina WTM Utility na wengine wenye mipango ya kitapeli tapeli tuwapige chini. Tusaidiane kujenga sio kuibiana.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 7:58:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Nakubaliana na wengi waliokwisha kutoa maoni yao.

Ila kwa wale walio Tanzania, napenda niwajulishe hili.. Uchumi wa nchi nyingi zilizoendela na Tanzania ni tofauti sana. Hivyo wakati mwingine ni ngumu kulinganisha kipata moja kwa moja.
Hebu tufanye 'rough' hesabu

Kama tutatumia exchange rate hii:
£ 1 = TShs 2400

Nauli ya 'daladala' London kwa trip moja ni £ 2 (kama huna Oyster, na £ 1 kama una oyster) ambayo ni sawa na TShs. 4800 ama TShs. 2400 za Tanzania. Daladala bongo ni kati ya TShs. 250-500 kwa trip.

Huo ni mfano wa kitu kimoja tu. Ingawa ni rahisi kutengeneza Pounds, lakini matumizi yake yako juu.

Pili, Watu wanaosave (mfano UK), wanajibana hasa, na wanafanya kazi masaa mengi kwa siku, na wainaishi kwa kubanana (wengi wao). Kama akili na nguvu na juhudi na heshima wanayotumia UK wakiitumia Tanzania, wanaweza kupata kipato kizuri tu.

Kurudi ama kutokurudi ni uamuzi wa mtu kulingana na uwezo binafsi wa mtu wa akili, nguvu, na mtizamo.

Ila jambo moja sio siri... Hakuna raia wa nchi yoyote ile (labda Tanzania), ambaye anapenda raia wa nchi nyingine.

Daniel, London


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:03:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Nampongeza sana mdaua alitoa hoja hii. Kwanza niseme kabisa baadhi ya watu waliochangia hoja hii wengi wao hawana degree yeyote nje ya Nchi, nasema hivi sababu nimesoma comments nyingine unaona kabisa mtu ameridhika kubaki hapa. Watu wengi walioridhika kubaki abroad ni wale ambao walikuja kusoma halafu shule ikawashinda au walikuja na student visa wakahamu kuingia mitihani. Kwa upande wangu natarajia kumaliza masomo yangu next year 2008 Masters in International relations baada ya hapo narudi nyumbani. Hapa Marekani ubaguzi siyo mwingi sana, lakini lazima waangalie watu wao kwanza, above all, nyumbani ni nyumbani tu. Thanks
Tim


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:06:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

mmh...Watanzania tuna kazi! Ukiangalia jinsi watu walivyo na wasiwasi na kutojiamini kuhusiana na kuishi huko home, utaelewa ni kwa nini nchi yetu inaongozwa na watu wasio na professions hata wanasiansa, na ni vipi kirahisi inavamiwana na watu wa nchi nyingine na wakaendelea kujinufaisha na kufaidika na nchi yetu. Wakati sisi bado tunajadili..nirudi au nisirudi! lakini kwa nini hatujiulizi, nchi za wenzetu tunazoishi zilijengwa na nani? hayo maji bwelele au umeme wa kila siku usiokatika uliletwa na nani?! Kama wazungu wa Uk, Us na nchi nyingine za magharibi wangeyakimbia matatizo ya nchi zao basi nani angeziondeleza nchi hizo..mpaka leo nasi tukakimbilia huko? Nchi za Kiafrika na Tanzania ikiwepo zaidi ya rushwa na matatizo mengine..tatizo kubwa zinazokabiliwa nazo ni kukosekana wasomi wa kutoa mawazo ya maendeleo na kutatua shida za jamii. Kwani kila siku maelfu ya wasomi wanaosoma nje wakipata tu vyeti vyao, wanazamia huko huko na kuogopa kurejea home na kusaidiana na wananchi wa kawaida kujenga nchi. Suala la kurudi au kutorudi nyumbani linategemea na mawazo ya mtu na jinsi anavyoijali jamii yake na nchi yake kwa ujumla. Ni kweli kiwango cha mishahara nyumbani hata kwa wasomi ni kidogo ikilinganishwa na nje, lakini wasomi haifai kufikiri mishahara tu..yapasa pia tujaribu kutumia uzoefu na usomi wetu kujaribu kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini tunaporudi ili kuweza kujiingizia zaidi hizo pesa na pia kusaidia kutatua matatizo ya kijamii. Mimi naishi nje ya nchi kama mwanafunzi, lakini kwa kufanya kazi ya part time na kazi ingine ya kusomesha lugha ya Kiswahili chuo kikuu ambayo haichukui muda wangu sana, mshahara wangu si mbaya. Lakini nimepania kurudi nyumbani na kuchangia kile nilichokipata kimasomo na wenzangu... Watanzania, lazima watokee ambao watajitolea ili nchi yetu nayo tuifanye kama za wenzetu..Nimeshapanga mipango yangu na nina matumaini kwa kutumia uzoefu na usomi wangu nitafanikiwa tu home :)
Shime wasomi tuijenge nchi!kwa ajili ya vizazi vijavyo
Kukata tamaa ni ndugu ya kifo!


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:13:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Wazee tuacheni imani potofu kwamba ukiwa Mtanzania basi maisha ni Tanzania tu. hii si kweli maisha ni sehemu yoyote pia tunasahau kwamba kazi ni kazi kwani wangapi hapo bong wanafanya vibarua na maish ayanakwenda, tatizo kubwa tulilonalo wabongo ni tunadharau kazi za watu. Mimi ni Kijana wa miaka 27 sasa nipo hapa UK nilimaliza Degree yangu ya Masoko 4 years ago. Nanilifanya hizo kazi ambazo mnazidhalau ie kuosha vyombo, mabox etc. Lakini sasa ninakampuni yangu binafsi japo ni ndogo lakini inazidi kutanuka siku hadi siku, nachotaka kusema ni kwamba ni watanzania wachache sana wenye focus na maisha especially hapa UK, mie huwa najribu naangalia sana wenzutu wa-nigeria mbona wao wanafanikiwa na wanfanya kazi proffessional na biashara binafsi. Watanzania tuache midomo tufanye kazi kwa bidii ili tufanikishe mahitaji yetu.
Asante sana kaka Michuzi kama utapost hii ujumbe

Mt Ltd London


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:37:00 PM EAT, Mtoa Maoni: mlalahoi

Mada nzuri sana hii. Mchango wangu:

uamuzi wa kurudi au kutorudi nyumbani ni wa mtu binafsi. Mimi uamuzi wangu ni huu
1) Nitabakia ughaibuni, ila ningependa kuja Nyumbani kutembea angalau kila mwaka
2) ajira na nafasi niliyonayo sasa hivi nimelizika nayo-mshahara, vitendea kazi n.k. na kama nikiichoka nitaacha na kutafuta kazi nyingine
3) swala la mbu, na malaria nalo ni kubwa mno kwangu -mie binafsi nashukuru kuwa huku ughaibuni sina haja ya kuwa na wasiwasi wa kupata malaria-ambao ni ugonjwa wa kutisha hasa ukipata watoto wadogo.
4) misiba mingi mno nyumbani
5) harusi nyingi mno-
6)gharama za elimu ya watoto zimepanda mno, bila pochi mtoto hapati elimu ya uhakika. Hapa nilipo (canada) mtoto anaenda shule ya uhakika bure!!
7) Kwa ufupi, ukilinganisha gharama za maisha za nyumbani (mfano pale Dar) nafikiri matumizi ni makubwa mno kuliko hata sehemu nyingi za ughaibuni. Jumlisha gharama za harusi, luku, misiba, ndugu, shule za watoto, petroli n.k. niambia kuwa maisha ni nafuu nyumbani kuliko ughaibuni. Mie nimeishi sehemu zote mbili sikubaliani na swala la kusema kuwa kuna unafuu wa maisha nyumbani kulinganisha na ughaibuni.
napenda kuwasilisha!!


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:39:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Mie simshauri mtu ambaye anaona ana kipato kizuri na kinamwingizia pesa nyingi arudi nyumbani, hapana ninachomshauri HIZO PAUNI AU DOLA ZAKE AKAWEKEZE NYUMBANI ili nasi tuendelee, kwa njia ya remittances kama kusaidia ndugu na jamaa, au kuwa na vitega uchumi au miradi ya maana ya kuweza kuwaajiri wengine na kuinua uchumi. Na mkijikusanya wengi mkawa na umoja wenu basi muwe mnachangia shughuli za maendeleo huko vijijini kama ujenzi wa shule, zahanati, upatikanaji wa maji safi na salama. Hapo mtakuwa mmefanya jambo la maana na mtakuwa na mchango mkubwa zaidi nyumbani kuliko kurudi. Tunataka mrudishe kile wakoloni walichukua kutoka kwetu (sijui kama itawezekana).

Serikali imeona umuhimu wa walio nje ya nchi kwa kuona mifano kama nchi za west africa (Senegal) ndio maana kuna mabadiliko ya sheria yanakuja kuruhusu uraia wa nchi mbili, ili nasi tunufaike na kuwepo kwenu huko nje. Ni njia nzuri pia ya kuingizia nchi kipato si mchezo kama kweli mtawekewa mazingiria mazuri na nyie mkaamua kufanya kweli mabadiliko nyumbani yatakuwepo, kaeni huko huko tunahitaji mchango wenu katika uchumi.

Kenya inapeleka watu kihalali kabisa kufanya kazi mpaka nchi za uarabuni, hamkusikia wale madereva waliotekwa Iraq kipindi kile? Leteni hizo dola huku ile shilingi istabilize maana hawa wahindi na wazungu waliopo huku wanazipeleka makwao


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:46:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Niko USA miaka saba. Toka nije huku siwahi pata kipele hata kimoja. Wala KUJIKUNA hata mara moja. Sijaona umeme umekatika, chakula cha kumwaga; sina haja ya kudhaminiwa na kampuni naweza kwenda nch yoyote duniani kutembea. In fact naenda Brasil in January kwa gharama zangu. Nitarudi bongo kusalimia tu; mbu, malaria, vumbi, foleni, etc. Cant take that.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 8:59:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Michuzi

wadau wapendwa,
sina kawaida ya kuingilia mada, hususan kwenye ukurasa huu ambao ni wenu. pia napenda kumpa shukurani na pongezi nyingi mchokoza mada kwani hakika naona amegota ikulu. vile vile nakaribisha mada ama uchokozi wa namna hii ili wadau tujadili kwa kina. pongezi zangu pia kwa waliochangia na ambao watachangia kwani hadi sasa tukiwa na michango 50 na ushee hakuna aliyepitiliza kwa kutumia lugha isiyofaa. nina furaha pia kuona kwamba utani wa kuitana 'wabeba maboksi' na 'wala vumbi' sio tu umetuweka pahala pa kuelewa huyu yuko wapi, ingawa ni kweli naungama kwamba sio wote ni wala vumbi ama wabeba maboksi popote walipotajika hivyo. kwa hiyo naomba tuendelee kuwa wacheshi na wavumilivu kwa kuitana hivyo kwani bila wenyewe kujua tumehajipigia mihuri ya utambuzi wa pahala mtu aliko.

najua wengi mtakuwa na hamu ya kujua nasimamia upande upi kati ya 'wala vumbi' na 'wabeba maboksi'. kwa idhini yenu na kwa unyenyekevu mkubwa naomba mniruhusu nibakie tu kuwa tarishi wenu na sio mwanachama wa upande wowote kati ya hizo pande mbili za vumbizzzz na boksizzzzz...

aluta kontinyua na hakuna noma wala nini wadau. na tuliendeleze hili libeneke la mjadala hadi kieleweke.


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 9:06:00 PM EAT, Mtoa Maoni: mdau

Mtoa mada ...
Kama woote walivyosema awali hapo ni bongo tumia akili yako uone how will you survive in the next 20 yrs .
Kuishi bongo kuna taabu yake na uzuri wake .starehe ni kibao ila nayo life span ni fupi huna uhakika wa kuishi zaidi ya miaka 70 wakati ukiwa nje una uhakika wa kuwa na long life span .
Huwezi kutumia elimu yako mpaka mwisho .. kazi bongo ni chache mno kustaafu nako nje nje tunawaona wazee wetu kibarua kikiota mbawa tu tayari anapagawa .. mapressure kibao mara ameanguka bafuni mara kule
basi karaha moja kwa mbili .. shamba la babu limeungua mara mtoto wa mjomba hajaenda shule
ili mradi tu ... mimi ninauhakika wa kupata 6 million Tsh per month ukitoa ghasia zoote niauwezo wa kusave 4Tsh ...nimeisave kwa muda wa miaka mitatu na sasa ninauwezo wa kutuma container mbili kila mwezi ambazo zinaniingizia 40 million per month hapo bado ni kijana mdogo tu wa 28 yrs ...sasa huo mshahara wa serikali wa 0.3 Tshmillion utadunduliza mpaka lini ufikie huo mtaji wangu si ndio chanzo cha kuomba rushwa , kusigne vocha feki kama Papaa Msofe ...
Kazi yangu naheshimiwa .. napata bonus yangu ya nguvu 3 times ya mshahara wangu mara mbili kwa mwaka . Je ni ofisi gani hapo bongo wanaweza kutoa motisha nzuri kwa wafanyakazi .
Ni wewe na akili yako tu wadau


Tarehe Wednesday, December 5, 2007 10:32:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Nirudi bongo?? Kufanya nini!! Sijazoea kulala saa 3 sababu umeme umekatika. Hata Bakhresa anakosa maji angalau ya baridi tu wakati fulani, mie napata ya moto 24/7. Bongo kazi huko ni kusubiri Miss Tanzania tu, ikiisha mwaka umeisha. Huku man, dola yako tu. Maisha mazuri mno.


From: Michuzi Blog

No comments: