Thursday, 14 June 2007

...nyumba jirani ...

Jaji mmoja mwandamizi amenusurika mvua (jela) baada ya kutuhumiwa kwa kosa la kum-flash mwana mama mmoja Oktoba 2006. Hakimu amesema kuwa mlalamikaji hakutoa ushahidi wa kutosha kutia hatiani mlalamikiwa.
Jaji mtuhumiwa huyo mkazi wa west London maeneo ya Wimbloden alituhumiwa kuwa ktk kipindi hicho Oktoba mara 2 alimvulia nguo za ndani dada huyo ndani ya treni. Ilibidi jaji atoe ushahidi kwa kutumia nguo yake ya ndani aina ya ck na kuonyesha ni jinsi gani ilivyo vigumu kumfunulia mtu maungo yake ya siri, tena ndani ya treni iliyojaa watu. Kwa hiyo huyo jaji alidai kuwa mlalamikaji alikosea kumtambua mtuhumiwa halisi (mistaken identity).
Baada ya hukumu Jaji na mkewe walifurahi na kusema sasa ataendelea na kazi yake kama kawaida maana jina lake limesafishwa.

No comments: