Ipo haja ya viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani nchini kuwemo ktk Bunge la Jamnhuri ya Muungano au Baraza la Wawakilishi.
Kwa hiyo napendekeza kuwa sheria husika zipitiwe ili viongozi wa vyama vinavyopata 5% au zaidi ya kura zote ktk uchaguzi Mkuu (wa Rais), waweze kuingia Bungeni moja kwa moja. Hii itaimarisha zaidi demokrasia yetu changa nchini. Au vyama vyenye sifa ya kupata ruzuku toka serikalini viweze kuwakilishwa bungeni na viongozi wao. Lengo ni kuimarisha demokrasia na kuvipa uhai 'zaidi' vyama vya upinzani.
Kwa maana hii, viongozi wa vyama vya CUF -Ibahimu Lipumba (na Maalimu Seif -wawakilishi Z'bar), Chadema -Freeman mbowe, TLP - Augustine Mrema wangeweza kuingia Bungeni moja kwa moja kwa kuzingatia matokeo ya uchaguzi Mkuu uliopita!
Natumaini Bunge lingepata msisimko zaidi!!!
Monday, 25 June 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment