Friday, 22 June 2007

Maoni: Mafao Kwa Wastaafu Tanzania*

Mheshimiwa Mzee J S Malecela.
Napenda kutoa pongezi kwa mchango wako bungeni kuhusu mafao kwa wastaafu. Nimefurahi hasa ulipoamua kuwa, pamoja na serikali kulifuatilia, wewe mwenyewe na wabunge kwa ujumla kuchukua jukumu la kuwaorodhesha majimboni ili mafao yao yashughulikiwe.
Ni matumaini yangu kuwa waheshimiwa mkishakabidhi orodha hizo, waziri atakeshughulia hizo orodha awe anatoa update ya malipo mafao hayo kila mara (hasa kila baada ya miezi 2 hadi 3) bungeni.
Hongera pia kwa mchango wako kuhusu kauli na kitabu cha Profesa Malyamkono -'the promise'. (Mimi) ninakuunga mkono kwani viongozi mlioweka msingi imara wa taifa hili ni vizuri kazi yenu itambuliwe na kuthaminiwa.
Nakutakia kila la heri.
Edison

*Hii ni barua yangu kwa Mheshimiwa John Malecela (MB Mtera, Makamo wa M/Kiti CCM Taifa) tarehe 28/9/2006

No comments: