Hongera kwa ushindi dhidi ya Juve, unajua ktk mchezo pamoja na vipaji, ufundi, nguvu, speed n.k. kitu kingine muhimu ni BAHATI. Safari hii Arsenal bahati imewaangukia.
Zipo bahati za aina nyingi mfano;
1. refarii na kipenga:
kupewa au kunyimwa penalti ktk mchezo, mchezaji kupewa au kutopewa red card, maamuzi ya utata kuhusu goli au kukataa goli n.k.
2. game:
ziko siku nzuri na mbaya ktk game lakini timu inashinda hata bila kucheza vizuri.
Kwa upande wenu Arsenal timu bado ni changa na bahati inawasaidia. Bado siamini kuwa mtafika fainali (au kuchukua kombe) kwa sababu hamna uzoefu.
Kuhusu mechi ya kesho Old Trafford, Man Utd itashinda. Uzoefu, Nguvu, Ushambuliaji wa Man U ni mkubwa kuliko Arsenal. Nafasi yenu kushinda au kuambulia sare ni ndogo sana.
Ktk kiungo hali yenu sio mbaya tunaweza kulingana. Ulinzi tunawazidi, Golini tuko sawa kwa hiyo washambuliaji + viungo ndio wataamua mechi - vitu ambavyo Man U ipo juu yaArsenal.
* Ujumbe huu niliuandika tarehe 08/4/2006, na maoni haya ni yangu binafsi kutokana na tathmini yangu ktk soka la Uingereza.
Hivi sasa mambo si shwari Arsenal na msimu uliopita nusura wakose hata nafasi ya 4 (champions league positon)!!
Thiery Henry nae uzalendo umemshinda kaona bora ajiondokee.
Hatma ya Arsene Wenger iko ktk hatihati huenda nae yuko njiani kuondoka Arsenal mwishoni mwa msimu ujao (mkataba wake utakapoisha)!!
Ujenzi wa uwanja mpya wa Emirates umeigharimu Arsenal hela nyingi na hivi sasa wanarudisha deni kwa wakopeshaji (creditors); ila hali itarejea shwari baada ya miaka 5 hivi. (Wenger aliwahi kusema, mwaka 2003, kuwa hali ya kifedha Arsenal itarejea ktk hali nzuri baada ya miaka 8 na hivi sasa imeshapita miaka 4 tangu kauli ya Wenger). Ndio maana Arsenal kwa sasa hawana hela ya kununua wachezaji wazuri ambao wanagharimu zaidi ya £15mil. Utaona mara nyingi wachezaji wa Arsenal wanagharimu chini ya £10mil. na sio kwamba wanapenda au kubana matumizi; jibu ni kwamba hawana hela za kushindana na timu za Man Utd, Chelsea na Liverpool. Na kwa sasa hata West Ham inawashinda Arsenal ktk soko la kununua wachezaji!!!
Ni lazima Arsenal iamue sasa kutumia hata kama ni kukopa zaidi au kumkubali owner mwingine ambae atawekeza hela zaidi.
Monday, 25 June 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment