Mawaidha kuhusu Ndoa Part II
SIFA ZA MWANAMKE (SIFA NJEMA)
1. Awe mwema - Mith 12:4, 31:10 -30
2. Mwenye hekima - Mith 14:1 16:5,24
3. Mwenye adabu - Mith 19:14, 11:16a
4. Mwenye busara - Mith 19:14
5. Awe mkarimu - Mith 22:9
6. Msafi (mwili na nyumba)
7. Mpole - Mith 15:1
8. Mwenye huruma
9. Mdadisi
10. Mvumilivu
11. Mcheshi (kiasi)Yampasa mke aanze siku kwa kauli nzuri hata kama anaumwa:-
- Amusalimie mume
- Amwage mumewe akimtakia kazi njema baada ya kumuandalia
(a) Maji ya kuoga
(b) Kifungua kinywa
(c) Nguo za kuvaa siku hiyo
Mume atokapo kazini:-
(a) Mkaribishe kwa tabasamu, mkaribishe kwa furaha.
(b) Mpigipige mgongoni
(c) Vaa nguo nzuri (mwanaume hupenda anachoona) macho huvutiwa kwa kuona
(d) Waeleze watoto wako unavyompenda baba yao ( watoto nao watawapenda wote)
(e) Kila mmoja wenu ajue kile anachopenda ua anachotaka
ILI KUMHESHIMU MUME
Muombee kila siku - Yeye alivyo hekima, busara, ulinzi, baraka, ujuzi, kuelewa, kiroho, mafanikio, kushinda majaribu nk - angalia na tarajia majibu ya maombi - Mshukuru Mungu kwa kazi anayofanya kwa familia yako - Mshukuru Mungu kwa ajili ya Mume wako- ombea mtazamo wako.
Kumbuka Mungu amemuweka mume wako kuwa kiongozi wa nyumba yako pamoja na wewe.
Angalia sifa za mumeo na uzikubali na ongeza mara kwa mara
Mwambie mumeo ni namna gani unamfurahia na kumpenda
Usitoe sifa zake mbaya mbele za watu au kubisha
Mtie moyo na kuwa msaaada wakati wa jambo gumuJihadhari na jinsi unavyomuuliza maswali
Changamkia pale anapoonesha upendo
Fikiria mambo mazuri juu ya mumeo
Thamini vitu anavyovipenda na asivyovipenda Mith 12:4
KAWAIDA MWANAMKE
Usitegemee starehe nyingi kama zile ulizokuwa unapata kwa wazazi wako au ndugu zako
Utakuwa na juhudi katika kujenga nyumba ya mume wako uliye naye. Mith 14: 1 Kila mwanamke aliye na heshima.......................
Hutakuwa mgomvi na mchokozi wala kumpiga mumeo kwa mwiko Mith 21:19
Utampa mume wako haki yake 1Kor 7:3-5
Thamani ya mumeo ni zaidi ya wanaume wote. Ez 16:32
Umtii mumeo kwa Roho ya upole na unyenyekevu 1Pet 3:1-4
Usimuruhusu mtu yeyote atambue kwamba unao wakati mgumu ( siri za ndani zisitoke nje) 1pet 5:9
Utahaakikisha macho yako yanamwangalia mumeo wakati amevaa kabla ya kutoka kwenda kazini au kutembea
Utajitoa na kumtii mumeo kwa moyo wote na kumruhusu kuwa kichwa cha nyumba Kol 3:18, 1pet 3:6, Ef 5: 33
Utahakikisha mumeo ni bora kuliko watu wengine Fil 2:3, Wimb 5: 9-16
Mwanaume ni dereva wa gari la ndoa na mwanamke anaweza akashauri na kupednekeza njia ya kupita na siyo kunyang'anya usukani
9. SIFA ZA MWANAUME
1. Mpole
2. Asiwe mwepesi wa hasira
3. Mcheshi
4. Anayeshaurika
5. Anayewajali watu wa nyumbani mwake (mahitaji)
6. Aliye na shukurani na kusifu (kwa lolote jema alilolitenda mkewe)
7. Anayeaga aondokapo kwenda matembezini au kazini au popote.
10. WAJIBU WA WA MUME KWA MKEWE
1. KUPENDA - kwa kiwango cha Kristo kwa kanisa Efe 5:25 matatizo mengi hutokea kwa sababu watu hawajui maana na jinsi ya kupenda kupenda ni matendo (action) siyo kujisikia au kuhisi ni kufanya vitu vizuri kama vile kutoa, kutabasamu, kusamehe nk Yohana 3:16
2. KIONGOZI (KICHWA) MTAWALA - Mume ni kichwa cha mke Efe 5:23 Naye atakutawala Mwanz 3:16c Amri hii hairekebiki kwa kelele za UWT kudai usawa ila utekelezapo maagizo ya Kristo amri amri ya kutawaliwa inakufa
3. MLINZI WA MKEWE - Kama chombo kisicho na nguvu, 1pet 3:7, Naye ni mwokozi wa mwili Efes 5:23 Mke hujiona salama awapo na mumewe Isay 4:1 Hivyo mume mlinde mkeo na maadui wa ndani na nje kama vile baba na mama, mashemeji/mawifi na marafik
4. KUTUNZA FAMILIA. Kuhakiki familia inapata chakula cha kutosha, malazi, mavazi na elimu kwa watoto Mwanzo 3: 17
5. KUMPAMBA MKEWE - mume sharti ampambe mkewe apendeze ili aweze kuvutia (amununulie vipodozi, nguo nk)
KAWAIDA MWANAUME:
Utamheshimu mke wako kama mrithi pamoja na wewe katika neema ya uzima katika Kristo Yesu. 1Pet 3:7
Mke wako ni mtu wa kwanza kwako siyo ndugu zako wala rafiki zako Mwanzo 2: 24 Mtaambatana na kuwa mwili mmoja
Mara kwa mara utamwambia mke wako alivyo wa muhimu na thamani kwako Fil 2:3 , Mith 31: 10,11
Utaendelea kumpenda kwa upendo ule wa kwanza wa wakati unampata. Wimb 5: m10 - 16
Utakuwa kiongozi wa kusimamia nidhamu ya nyumba yako ukisaidiwa na mke wako. Efes 6:4
Utakumbuka kutekeleza au kutimiza vile vitu vidogo ambavyo ulimwahidi mke wako kwamba utafanya Math 5: 37
Macho yako yataelekea kwa mke wako tu na sivinginevyo. Mith 5: 15-20, Ayub 31:1, Yer 5:8
Utafanya juhudi kusikiliza yale yaliyosemwa na mke wako. Mwanz 21:12
Utambusu kila siku asubuhi kwa upendo. Wimb 8:1
Hutakuwa mchungu likija swala la fedha. Est 5:3
12. WAJIBU WA MKE KWA MUMEWE KUTII - Kumtii mume kama kumtii kristo Bwana Yesu efe 5:22 watu huchanganya sana neon kutii na kuheshimu. Kutii kunakosemwa hapa ni kuwa endapo wawili mume na mke mmeshindwa kufikia uamuzi wa pamoja, basi,basi mke atatii uamuzi wa mumewe kama vile wamekubaliana awali
KULEA WATOTO (FAMILIA)
(a) Kuhakikisha afya ya mumeo na watoto
(b) Kuhakikisha kuwa chakula kinaliwa kwa wakati na kizuri
(c) Kuhakikisha usafi wa malazi, mavazi na miili yao
(d) Kufundisha watoto maneno ya Mungu
(e) Kuchunguza nyendo na tabia za watoto na mumeo na kuchukua tahadhari mapema.
KUMSHAURI MUMEO
Mke mwenye busara ni mshauri mwema kwa mumewe. Hatatoa ushauri wa kuleta maangamizi. Ushauri unafaa lakini ushauri mwingine upimwe kabla ya kufanyia kazi. Ona mashauri mabaya ya wanawake kwa waume zao
(f) Hawa kwa Adamu - Mwanza 3:17 (kula tunda)
(g) Sara kwa Ibrahimu - Mwanzo 16: 1-3 kulala na mjakazi (tabu ya mashariki ya kati)
(h) Yezebeli kwa mfalme Ahabu - 1Falm 21:22/2Falm 9:10
(i) Zereshi kwa Hamani mumewe kwa habari ya Mordekai Esta 5:14, 7:9-10
(j) Mkewe Ayubu kwa ayubu mumewe - Ayubu aliukataa ushauri wa mkewe. Ayubu 2:9
13. ADUI WA NDOA NI:-UTAJIRI - Tajiri hupendwa na wasichana na pia huwa na tamaa ya kutafuta fedha kiasi cha kukosa muda na mkewe
UMASKINI - kazi ya kutafuta lishe ni ya baba, hivyo hushughulika sana na kujikuta amekuwa baba zaidi kuliko kuwa mume
MADARAKA - madaraka ya ofisini huyaleta hadi nyumbanini chukuzo kwa mume/mke. Maafisa hawana muda na wake zao kwa sababu ya makongamano/semina/ziara mbalimbali.
- Hivyo wake zao wengi hutumia madereva kukidhi haja zao za kimwili
- Mke ambaye ni ofisa humwachia house girl kazi za kupika, kufagia chumbani, kupeleka maji bafuni na hata kutandika kitanda, hivyo kusababisha mke kupinduliwa na house girl.
MAMBO YANAYOWAKERA WAKE ZETU
Wababa wenye madaraka kuyapeleka madaraka nyumbani
Wake kuwajibika na mambo ya nyumbani kwa vile wana mishahara minono
Wababa kutotenga muda wa kutosha kukaa na wake zao ili kuongea yanayowahusu
Mume kumwachia mke kulea watoto hasa wakati wa usiku
Mume kutomtia moyo mke wakati wa ujauzito
Mume kumchanganya mama na watoto wa kike wanapokosa
Mume kutokuwa na maandalizi mazuri wakati wa kukutana kimwili na mkeo
Mume kujijari mwenyeweMume kusaidia ndugu zake bila mke wake kujua
Mume kubagua watoto
Mume kuwa na upendo na ukaribu au kucheka na binti waishio nao huku yupo mke wake
Mume kutomshirikisha mkewe katika huduma yake ya ili aweze kumwombeaKutoonesha shukrani wala kutokuwa na msamaha
Mume kutomtazama mkeo usoni mkiwa chumban
iMume kuongea kiutani na wanawake wengine mkeo akiwa hayupo.
posted by Chemi Che-Mponda at 1:50 PM
(From: Chemi's Blog)
Thursday, September 13, 2007
Ujumbe kutoka Kaka Lazurus Mbilinyi 'Mawaidha kuhusu Ndoa'
Wapendwa wasomaji nimepata ujumbe huo kutoka kwa Kaka Lazarus Mbilinyi ambaye aliandika somo la NDOA NA UNYUMBA ambayo umeisoma kwenye blog hii:
http://swahilitime.blogspot.com/search/label/Mbilinyi
**************************************************************************
Dada Chemi,
Mimi ndo Lazarus Mbilinyi niliyeandaa hilo somo la ndoa na nyumba na kwa bahati mbaya nilikuwa sijui kama linaweza kusomwa na mtu yoyote kwani katika kuliandaa niliandaa katika mazingira ya Tanzania na hasa vijijini na sehemu ambazo mwanamume anafanya kazi (ameajiriwa) na mwanamke ni mama wa nyumbani (anayejishughulisha na kazi zingine) na pia limeegemea zaidi katika familia za kikristo.
Naamini maoni ninayopata kutokana na hilo somo basi nitayafanyia kazi na kama inawezekana siku nyingine nitoe kitabu cha Ndoa na nyumbaHata hivyo nashukuru sana kwa kueneza ujumbe kwa watu wote ili wajue ndoa ni nini hilo nashukuru.
Kwa sasa nipo Canada kwa ajili ya shule niemfika hapa tarehe 1 Sept 2007 na naamini tutazidi kuwasiliana na pia nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu.
Asante sana kwa kazi njema ya kuelimisha jamii:
Lazarus P. Mbilinyi
Labels: Mbilinyi, Ndoa, Unyumba
posted by Chemi Che-Mponda
source: Chemi's blog
Friday, 7 September 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment