Tuesday, 11 September 2007

Bibi harusi afumaniwa

Aibu tupu Bongo! Bibi harusi afumaniwa

11 Sep 2007
By Mwandishi Wetu, Singida

Yale matukio ya aibu ambayo mara nyingi tulikuwa tukiyasikia kwenye nchi za wenzetu, sasa yameanza kuingia hapa kwetu Bongo na kuzua aibu kubwa!

Hebu fikiria, bibie ambaye ndiyo kwanza amefunga ndoa, anabambwa laivu na mumewe akijinafasi na bwana mwingine!

Tukio hilo la aibu lilitokea huko katika kijiji cha Kidaru, wilayani Iramba mkoani Singida.

Baada ya Bibi harusi huyo kukutwa akifanya aibu hiyo, inadaiwa mumewe alipata uchizi na kuamua kumcharanga mapanga kisogoni hadi kumuua.

Tukio hilo ambalo lilibadilisha sura ya maisha yao, lilitokea siku tano tu baada ya ndoa yao kufungwa.
Shauri hilo lilishafikishwa mahakamani na kwa vile mtuhumiwa alikiri kosa lake , likaenda haraka haraka na kutolewa hukumu.

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, ilimhukumu bwana huyo, Daud Yessaya, 46, kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukiri kosa la kumuua mkewe kwa panga.

Mshtakiwa huyo alimuua mke wake, Elizabeth Mkumbo baada ya kumfumania akifanya mapenzi na mwanaume mwingine siku tano tu baada ya ndoa yao.

Awali ilidaiwa kuwa mume huyo alimuona mkewe akiongea na mwanamume mwingine ambapo baadaye waliondoka pamoja.

Iliendelea kuwa mume aliamua kufuatilia nyendo zao ambapo baadaye aliwakuta laivu wakifanya tendo la ndoa.

Ilidaiwa kuwa baada ya kuwafumania, mshtakiwa aliamua kuchukua panga lililokuwa jirani na watu hao na kuanza kumshambulia mwanamme huyo lakini hata hivyo alikwepa na kukimbia.

Ilidaiwa kuwa panga hilo baada ya kumkosa mbaya wake, alimgeukia mkewe na kuanza kumkata kisogoni hadi alipokata roho.

Akitoa huo, Jaji alisema mahakama yake imezingatia ombi la wakili wa mshtakiwa huyo kwamba mazingira ya mauaji yaliyosababisha mshtakiwa atende kosa hilo.


* SOURCE: Alasiri

No comments: