Tuesday, 11 September 2007

Eti Uwanja wetu ni bomu??

Nimesikia kuwa viti vya uwanja wa Taifa vinang'oka na koki za maji chooni ni ngumu! Inaonekana miundombinu ndani ya uwanja ina mshikeli. Hayo yalitokea ktk mechi dhidi ya Msumbiji!!

Ifuatayo ni habari kutoka tovuti ya JamboForum yenye madai hayo!

uwanja mpya ni bomu....!
Ilisikitisha sana wakati magazeti yalipoandika kwamba watanzania wamepanda juu ya viti na kufanya vinyofoke. Hiyo ilikuwa kwenye mechi ya kwanza kuchezwa uwanjani hapi kati ya Tanzania na Uganda!
Ukweli niliushudia mimi mwenyewe kwa macho yangu siku ya mechi ya pili kuchezwa uwanjani hapo kati ya Tanzania na Msumbiji. Watazamani waliokuwa wamekaa kwenye "row" ya mbele yetu, viti vyao vilivyofoka toka kwenye zege ya uwanja huo bila ya wao kuwa wamefanya chochote. Walikuwa wamekaa wametulia, na hata mpira ulikuwa hauja anza!
Wachina wale waliotujengea uwanja mpya wana sifa ya kuwa na vitu vilivyo chini ya ubora na hili linajulikana dunia nzima! Koki za mabomba vyooni nazo baadhi yake ni ngumu sana kufunguka kiasi cha kuhitaji kutumia nguvu! Matokeo yake koki zinang'oka!
Mkandarasi mkaguzi wa serikali yetu aliyepewa dhamana ya kukagua na kuhahakisha ubora wa uwanja huo anatakiwa awajibike kabla uwanja huo haujakabidhiwa rasmi kwa serikali.
Kama watu wamekaa tu vitini, na vinanyofoka, tena toka kwenye zege, itakuwa wakiwa wanashangilia na kucheza uwanjani? Yatakuja kutokea maafa ya karne ndani ya uwanja ule siku moja endapo tahadhali hazitachukuliwa!
Tuache kuwasingizia watanzania kwamba ni waharibifu! Nimekereka!
Source: JamboForum, 10/9/2007

Hivi karibuni nilitoa maoni yangu kuhusu huu uwanja, leo nakumbushia nilichokisema mwezi uliopita.

Ni jambo la kujivunia sana kwa nchi yetu kujipatia uwanja wenye hadhi ya kimataifa. Naupongeza uongozi ktk serikali ktk kusimamia kidete sera ya michezo kwani bila uwanja murua michezo haiwezi kukua au kuvutia kizazi kipya cha wanamichezo nchini. Pia tuaweza kuomba na kuandaa mashindano makubwa kwa kuwa tuna miundombinun safi ambazo ni kigezo cha kupewa michezo yeynye hadhi ya juu.
Kutokana na umuhimu huo na sifa za uwanja wetu, ninayo machache ningependa kuyaweka hadharani ili wenye dhamana wna uwanja waweze kunisaidi au kuisaidia jamii nzima ya watamzania wenye dukuduku kama langu!
Bila shaka wahusika wataweza kunisaidia ktk kuondoa hili dukuduku.
Napenda kuanza kwa kuuliza kama uwanja wetu wa Taifa una sehemu ya biashara ya vinywaji na vyakula (kwa ndani) wakati wa mapumziko au kabla ya mechi kuanza. Natoa rai kuwa tujifunze kupitia wenzetu wenye viwanja vikubwa ktk sehemu mbalimbali duniani, mfano uwanja wa Wembley.
Wembley wanaingiza sana hela kwa biashara ya vinywaji (soda, juisi, maji baridi hata pombe) na vyakula kama chips, mayai, piza, burger, sausage n.k. Biashara hufanyika kabla mechi kuanza na wakati wa mapumziko au wakati wa matamasha mbalimbali yanayofanyika Wembley.
Ningependa kuona utawala wa uwanja wa Taifa wanaweka huduma kama hizi maana zitaingiza fedha nyingi sana mbali na viingilio vya mlangoni.
Hata hivyo kuwepo na kutokuwepo kwa huduma hizi kutategemea sana usanifu wa awali wa uwanja wenyewe. Pia itategemea kama wenye uwanja nao walihitaji huduma za kibiashara kujumuishwa ktk usanifu/ujenzi wa uwanja.
Ninapoutazama uwanja wa taifa ktk picha naona kama vile ni kwa ajili ya michezo tu na hakuna nafasi ya sehemu za biashara au kumbi za mikutano!
Kwa upande mwingine nina dukuduku au maswali ningependa kuwauliza wenye uwanja wa taifa.
Ningependa kuuliza kama utawala wa Uwanja mpya wa Taifa na halmashauri ya Manispaa Temeke wameshafanya majaribio ya kuutumia uwanja kabla ya mechi rasmi!
Mfano Wembley ulipokamilika ulihitaji leseni ya kuendesha mechi na matamasha kutoka halmashauri ya mji wa Brent ambapo uwanja upo.
Kabla ya kupewa leseni Wembley walitakiwa wafanye majaribio, na waliandaa mechi 2, ambapo watazamaji waliingia bure na watazamaji waliombwa waingie vyooni karibu wote (kuna vyoo vingi sana ndani ya wembley) na ku-flashi maji ya chooni kwa pamoja, ktk muda mmoja, ili ku'test' drainage ya maji machafu uwanjani, pia walikaa vitini na kuruhusiwa kurukaruka na kushangilia kwa vishindo.
Baada ya test hizo 2 ndipo maafisa wa Brent walikagua uwanja na kuridhika kuwa 'health and safety' standards/regulations zimezingatiwa na hivyo kutoa leseni.
Hapo ndio mechi za England vs Brazil n.k. zikafuata.
Ulinzi ktk uwanja pia ni muhimu sana hasa kwa kuhakikisha watazamaji hawaingii uwanjani na silaha au chupa za glasi ambazo zaweza kutumika kama silaha wakati wa harakati za kiushabiki.
Ulaya kuna utaratibu wa ulinzi na usalama ambao ni 'uniform' unatumika ktk viwanja vyote vya soka. Ni vizuri na sisi tujizatiti kuhakikisha vurugu tunazoziona ktk viwanja vya nje hazitokei kwetu, na kupunguza au kutokomeza kabisa vitendo vya kihuni uwanjani.
Mojawapo ya taratibu za viwanja vya ulaya kwa sasa ni kwamba vinywaji uwanjani huuzwa ktk glasi za plastic ambazo ni 'disposable' (vinywaji ktk 'cans' ni marufuku!! Au vinywaji vinakuwa ktk chupa za plastic ambazo kabla shabiki hajaingia uwanjani ni LAZIMA afungue chupa na kuacha mfuniko ktk lango ambapo walinzi huvikusanya vifiko hivyo. Hii maana yake ni kwamba endapo fujo itatokea na chupa ya plastic isiyo na mfuniko ikatumika kama silaha haiwezi kuleta madhara kama vile ingekuwa imefungwa na kifuniko au kama ingekuwa ya glasi.
Utaratibu kama huu ni mzuri na muhimu sana, ndio maana napenda kujua kama huko kwetu kitu kama hiki kimefanyika ili kuepusha maafa yasiyotegemewa!!
Uwanja upate MOT kwanza kabla ya mechi na Msumbiji!
Jambo jingine ambalo mimi linanishangaza ni kuwa uwanja wetu utatumia nyasi za bandia! Kwa kweli Tanzania hatuna sababu ya kutumia nyasi bandia maana hali ya hewa nchini (climate) inaruhusu nyasi kukua kwa mwaka mzima!
Specifications nyingine ni za ajabu na hii inatokana na kutumia wasanifu wanaotokea nchi zenye mazingira na hali ya hewa tofauti na sisi!
Ndugu zangu ninavyojua ni kwamba kuna nchi ambazo ni za barafu, majangwa au viwanja vya ndani ambavyo mwanga wa jua haliingii kiwanjani hapo ndipo nyasi bandia hufikiriwa/kutumiwa.
Kwa taarifa tu ni kwamba nyasi bandia zinaathiri uchezaji mpira na ankles za wachezaji (rejeeni ripoti ya mechi ya Celtic vs. Spatak Moscow wiki iliyopita) au fuatilieni mechi ya Russia vs. England ambayo itafanyika ktk uwanja huo wenye nyasi bandia!
Mpaka sasa waingereza wanalalamika sana mechi hiyo kuchezwa ktk nyasi bandia.Hatuna sababu kutumia nyasi bandia jamani!Vitu vingine havina maana kuiga eee!
Na Mosonga 23/8/2007

No comments: