Mapato ya Uwanja wa taifa yangeliweza kuwa zaidi endapo wenye uwanja wangefikiria kujumuisha huduma nyinginezo hapo uwanjani kama nilivyopendekeza ktk moja ya maoni yangu hivi karibuni:
Napenda kuanza kwa kuuliza kama uwanja wetu wa Taifa una sehemu ya biashara ya vinywaji na vyakula (kwa ndani) wakati wa mapumziko au kabla ya mechi kuanza. Natoa rai kuwa tujifunze kupitia wenzetu wenye viwanja vikubwa ktk sehemu mbalimbali duniani, mfano uwanja wa Wembley.
Wembley wanaingiza sana hela kwa biashara ya vinywaji (soda, juisi, maji baridi hata pombe) na vyakula kama chips, mayai, piza, burger, sausage n.k. Biashara hufanyika kabla mechi kuanza na wakati wa mapumziko au wakati wa matamasha mbalimbali yanayofanyika Wembley.
Ningependa kuona utawala wa uwanja wa Taifa wanaweka huduma kama hizi maana zitaingiza fedha nyingi sana mbali na viingilio vya mlangoni.
Hata hivyo kuwepo na kutokuwepo kwa huduma hizi kutategemea sana usanifu wa awali wa uwanja wenyewe. Pia itategemea kama wenye uwanja nao walihitaji huduma za kibiashara kujumuishwa ktk usanifu/ujenzi wa uwanja.
Ninapoutazama uwanja wa taifa ktk picha naona kama vile ni kwa ajili ya michezo tu na hakuna nafasi ya sehemu za biashara au kumbi za mikutano!
Ikumbukwe wenye uwanja wana deni la kulipia mkopo wa ujenzi wa uwanja huo, na hiyo mbinu ya kupata mapato ya ziada ingesaidia ulipaji deni kwa haraka zaidi!
Habari hii hapo chini ni kwa hisani ya blogu ya issamichuzi:
MECHI YA TAIFA STAAZ NA MSUMBIJI JUMAMOSI ILOPITA ILIINGIZA JUMLA YA SH. MILIONI 605, 020, 000/- KUTOKANA NA WATAZAMAJI 55,514 WALIOINGIA.
1. VIP 'A' WALIINGIA WATAZAMAJI 743 WALIOLIPA 50,000/- KILA MMOJA NA KUPATA JUMLA YA MILIONI 37, 150, 000
2. VIP 'B' WALIINGIA WATAZAMAJI 1973 AMBAO WALILIPA 40,000/- KILA MMOJA NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 78, 920, 000/-
3. VIP 'C' WALIINGIA WATAZAMAJI 2, 242, 000/- AMBAO WALILIPA 30,000/- NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 67, 260, 000/-
4. UPANDE WA RANGI YA CHUNGWA MYOOKO WALIINGIA WATAZAMAJI 5, 326 AMBAO WALILIPA 20,000/- NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 105, 520, 000/-
5. UPANDE WA CHUNDWA MPINDO WALIINGIA WATAZAMAJI 7,300 AMBAO WALILIPA 10,000/- NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 73,000,000/-
6. NDE WA MDUARA WA BULUU WALIINGIA WATAZAMAJI 18,340 AMBAO WALILIPA 10,000/- NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 183, 400, 000
7. UPANDE WA KIJANI A.K.A KAJAMBA NANI WALIINGIA WATAZAMAJI 19, 590 AMBAO WALILIPA 3,000/- NA KUPATIKANA JUMLA YA MILIONI 58, 770, 000/-
KWA MUJIBU WA MWEKA HAZINA WA TFF SILAS MWAKIBINGA ALIYETOA TAARIFA HIZI, MAPATO HAYO NI ASILIMIA 94 YA UWEZO WA UWANJA KWA KIINGILIO KILICHOWEKWA.
NAOMBA KUWASILISHA
(source: issamichuzi blog)
Thursday, 13 September 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment