Tuesday, 19 May 2009

Umuhimu wa maktaba

19/05/2009
Mbali na kutenga maeneo ya bustani za kustarehe ktk miji na vitongoji, maktaba ni sehemu murua pia kwa watu kupumzika huku wakijisomea vitabu magazeti na kupitia mtandao wa kompyuta.

napendekeza kuwa kila kata nchini iwe na maktaba yake kwa manufaa ya wananchi. Ipo kasumba kwamba baada ya masomo ya elimu ya msingi au sekondari basi hakuna tena kusoma au kujisomea.

Maktaba zinasaidia kuwafanya watu wawe na nguvu (active) hasa kutokana na kuchamsha ubongo ambao ndio dereva wa shughuli zote za viungo vya mwili. Akili ikichangamka mtu hupata furaha lakini ikidumaa mwili huchoka na kuweza kukata tamaa haraka.

Pia maktaba ni sehemu ya watu kukutana na kujuliana hali, kitu muhimu sana ktk jamii.

Watoto wetu pia watapata nafasi kujisomea, kujifunza pamoja au kucheza na wenzao wakutanapo maktaba. Na maktaba zinapokuwa karibu na maeneo tunayoishi inakuwa rahisi kwa kila mmoja wetu kuzitembelea kwa vile hakuna haja ya kusafiri masafa marefu (kitu ambacho hukatisha tamaa kwa wengi wenye nia ya kujiendeleza au kupata huduma za husika)

No comments: