-Ilikuwa tarehe 30/10/2007
watani wa jadi simba na yanga leo wamezabwa faini ya shilingi 500,000 kila mojakutokana na timu hizo kufanya vurugu wakati wa mechi yao iliyochezwa Jumatano iliyopita mjini Morogoro.
katika mchezo huo ambao Simba ilishinda bao 1-0 mashabiki wa Yanga waliwekavizuizi vya viti kwa lengo la kuzuia magari ya viongozi wa Simba nawachezaji tukio ambalo lilisababisha kushambuliwa kwa mawe, chupa za maji navimiminika vingeni gari la wachezaji wa Simba na mchezaji Haruna Moshialijeruhiwa.
yanga imepigwa faini ya shilingi 500,000 na imetakiwa kulipa gharama za uharibifu uliotokana na vurugu hizo ikiwa ni pamoja na matibabu ya mchezaji Haruna Moshi baada ya kuwasilishwa na kuthibitishwa na tff.
simba, ambao nao walihusika na vurugu kwa kurusha mawe, chupazilizojaa maji na vimiminika vingine na kusababishwa mchezo kusimama nayo imetozwa faini ya shilingi 500,000 na faini hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 31(1) na 66 ya tff.
......................................................
Maoni:
Tarehe October 30, 2007 9:11 PM, Mtoa Maoni: MOSONGA
Hiyo sheria ifanyiwe marekebisho haraka sana.
Sh 500,000/= haiwaumizi hawa simba na Yanga! Inatakiwa iwe sh. mil.5 as a minimum ili iwe fundisho!
........................................................
source: Michuzi | Monday, October 29, 2007
Friday, 29 May 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Sua yasambaza mbegu za teknolojia ya chupa
CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA)kimefanikiwa kuzalisha miche ya mbegu mbalimbali kupitia teknolojia ya chupa.
Teknolojia hiyo imewezesha kuzalishwa kwa wingi miche ya migomba, Vanilla na matunda ya mananasi. Uzalishaji huo imewezeshwa kupatikana kwa wingi wa mbegu za migomba aina ya Bukoba , Mzuzu , mshale na mbegu mpya pia zimepatikana na kuitwa kitaalamu kwa majina ya FHIA 17 na FHIA 23.
Mbegu za mananasi zinazozalishwa ni Queen Victoria na Smooth Kayene. Mratibu wa Kitengo cha Sayansi ya mimea wa SUA, Dk Deodous Msogoya amesema mbegu hizo ni matokeo ya kazi nzito ya utafiti kwa kutumia chupa na miche hiyo imesambazwa kwa wakulima wa mikoa ya Mbeya, Pwani na Morogoro.
Uzalishaji wa miche ya migomba na nyingine kwa kutumia njia ya chupa ulianza mwaka 2006 , ambapo katika kipindi cha miaka mitatu mradi huo umezambaza miche ya migomba bora zaidi ya 20,000 kwa wakulima wa wilaya nne za kutoka kwenye Mikoa mitatu nchini.
Wakulima walionufaika na miche hiyo ni kutoka kijiji cha Mwalusembe, Mkenge na Kimanzichana kwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, wengine ni wa kijiji cha Kyimo, Bujera, Katabe na Mbambo kutoka Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Aidha wakulima wengine wanaonufaika na miche hiyo ni kutoka kijiji cha Tangeni na Hembeti vilivyopo katika Wilaya ya Mvomero na wengine ni wa kijiji cha Pangawe na Kiroka wa Wilaya ya Morogoro.
Hata hivyo alisema mahitaji ya miche hiyo kwa sasa ni makubwa zaidi tofauti na mradi huo uliopanza kufanya kazi zake na hivyo ni kutokana na wakulima kutambua kuwa mazzo hayo yanafaida kubwa katika kukuza uchumi wao.
posted by Msimbe @ 10:46 AM 1 Comments
............................................
1 Comments:
At April 28, 2009 2:10 PM , MOSONGA RAPHAEL said...
Hizi ni habari njema. Hongera sana Sokoine Uni kwa utafiti huu............................................
source: lukwangule.blogspot.com Tuesday, April 28, 2009
Nilichosema: 05/05/2009
Leo, siku kuu ya wafanyakazi duniani, napenda kuwakumbuka wabeba boksi. Hao ni waTanzania wanaoishi ughaibuni, wakifanya kazi za mikono, kama vile kubeba na kupanga mizigo ya bidhaa madukani, kusafisha maofisi, kusafisha vyombo mahotelini, kuwatunza wazee, na kadhalika. Watanzania wanaposema kubeba boksi, wanamaanisha kazi za aina hiyo. Na jina hilo linatokana na huu kweli kuwa wengi wa wahusika wanabeba na kupanga maboksi.
Wabeba boksi wanataniwa sana katika jamii ya kiTanzania. Wabeba boksi wengi nao wanajitania. Watanzania wengi wanaziona kazi za boksi kuwa ni kazi duni. Napenda kubadili mtazamo huo kwa kuelezea umuhimu wa boksi. Natumia hilo neno boksi kwa sababu linatumika pia kumaanisha kazi ya kubeba boksi.
Jambo moja la msingi ni kuwa wabeba boksi wanatumia nguvu zao kujipatia kipato. Wao ni tofauti na wezi au mafisadi, ambao wanakula jasho la wenzao. Kwa msingi huu, mbeba boksi anastahili heshima.
Kila kazi halali ina umuhimu wake katika jamii, iwe ni kilimo, uvuvi, usafishaji vyoo, ualimu, udaktari, au upigaji muziki. Kila kazi ya aina hiyo inastahili heshima. Mpiga boksi anafanya kazi muhimu. Bila yeye, jamii itakwama. Anastahili heshima.
Wabeba boksi, kama vile walivyo waTanzania wengine wanaoishi ughabuni, wanatoa mchango mkubwa katika kipato cha Taifa, kwa hela wanazotuma nyumbani, iwe ni kwa ndugu, jamaa, marafiki, au taasisi. Nimesoma taarifa kuwa mwaka 2008, kwa mfano, watu hao waliliingizia Taifa dola zaidi ya 100 millioni. Wenzetu waKenya wanaoishi nje waliingiza nchini mwao dola zaidi ya 400 millioni. Ni wazi kuwa mbeba boksi, akiwa ni mmoja wa watu hao, ni mtu muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Je, lipi bora zaidi: kukaa vijiweni nchini bila ajira, au kubeba boksi? Hili ni suali la kutafakariwa.
Kuna wabeba boksi ambao, baada ya kukusanya hela, wanaanzisha miradi nyumbani wakiwa bado ughaibuni, na wengine wanarudi nyumbani na kuanzisha hiyo miradi. Kwa njia hiyo, wanatoa ajira kwa wananchi wenzao.
Mpiga boksi, kwa kukaa ughaibuni, anajifunza mengi. Anarudi nchini akiwa na upana wa mawazo kuhusu dunia na uzoefu wa nidhamu ya kazi, vitu ambavyo vinaweza kutoa changamoto kwa wananchi wengine.
Kwa ufupi, boksi lina umuhimu na heshima yake.
source: mjengwa blog, 05/05/2009
Comment: 3
Date: Tue May 05, 09:44:00 AM EAT, Anonymous
Nakubaliana nawe sana profesa. Siyo tu kwasababu niko ughaibuni, bali nikwasababu ya namna ulivyoeleza ukweli.
Huyo wanayemwita mbeba box, kwa nchi za wenzetu anapata malipo halali. Mianya ya wizi kama ilivyo kwa mafisadi au vibaka kule nyumbani, haipo huku nje. Kwa hivi siku zote anakuwa mtu wa nidhamu ya kazi na kufikiria kubadili maisha ya nyumbani -Tanzania.
Ukiacha tu hilo, mbeba box huku ughaibuni ana kipato kikubwa kumpita profesa wa chuo kikuu pale kwetu Tanzania (niwieni radhi kwa hilo, ni ukweli). Si wapiga boxi wote wanaopata fedha nyingi, lakini wanatengeneza hela nzuri kuliko zile ambazo wangepata nyumbani. Maisha ya mwezi mmoja huku nje yana kipato cha mwaka 1 au zaidi kwa huyohuyo mpiga boxi, iwapo atalinganisha na Tanzania.
Wapiga boxi, heshima sana kwenu!
Date: Tue May 05, 03:44:00 PM EAT, MOSONGA RAPHAEL
Naunga mkono maoni ya Prof Mbele na mtoa maoni hapo juu!
Hela ya mbeba box ina mzunguko mrefu ktk jamii yetu: hela ikitumwa; anayeenda kuipokea w/union anapanda daladala (kwa mfano), anakunywa soda njiani, akirudi anapitia mboga na kununua mahitaji ya nyumbani, kama ni mradi wa ujenzi atanunua saruji bati mchanga n.k. pia atamlipa fundi ujenzi. Hao wote waliopokea hii hela wataitumia kwa mahitaji yao anuai kama vile shuleni (karo au michango mbalimbali), hospitalini, kusafiri (nauli), mavazi, kuingia uwanjani/kumbini kuangalia burudani, na hata kufanya mahari kuolea mchumba!!
Kwa hiyo mbeba box ana nafasi kubwa sana ktk kuinua maisha, ustawi na uchumi wa wanajamii nchini.
Date: Tue May 05, 05:55:00 PM EAT, Anonymous
KWANI KUBEBA BOX SIKAZI KAMA ZINGINE ILA WATU KUPENDA KUDHARAULIANATU.SAWA NA KULIMA ,KUFUGA,KUVUA NA MAMBO MENGINE YALIYO YA HARARI
source: mjengwa blog, 05/05/2009
Wednesday, December 05, 2007
Ivo, Nsajigwa waomba radhi wanachama
Kipa namba moja wa Yanga, Ivo Mapunda na beki, Shadrack Nsajigwa wamewaomba msamaha wanachama wote wa klabu ya Yanga kutokana na makosa waliyofanya na kuwabembeleza viongozi wao wawarejeshe katika kikosi cha timu hiyo.
Wachezaji hao ambao walifungiwa kutokana na kuondoka kambini bila ya kutoa taarifa walisema hayo jana wakati wanazungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la soka nchini, (TFF).
Ivo alisema kuwa lengo la kuamua kuomba radhi ni kutokana na kuamini kuwa kosa walilofanya ni la kibinadamu na wao kama wachezaji wanategemea soka ili kujiendeshea maisha yao.
Alisema kuwa wamefikia maamuzi hayo kutokana na kufahamu kuwa wao ni sehemu ya maendeleo ya mpira hapa nchini na hivyo kutocheza kunawaathiri wao na nchi pia.
`Tunaomba msaada kwa wana- Yanga wote watusamehe makosa tuliyofanya, tuko hapa kwa ajili ya maendeleo,` alisema Ivo. Aliongeza kuwa mbali na kuondoka kambini bila ya ruhusa hakuna jambo lingine walilolifanya ikiwemo tuhuma za kuihujumu timu yao katika mechi yao na watani, Simba ambayo ilimalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0.
Inawezekana mambo ya kuchukua fedha yalikuwepo lakini mimi binafsi sijawahi kupokea fedha kutoka kwa mtu yoyote, alisema Ivo na kuongeza kuwa hawakucheza chini ya kiwango kama inavyosemwa na baadhi ya wana-Yanga.
Aliongeza kuwa tayari wameshaandika barua kwa viongozi wao na wanasubiri maamuzi kutokana na maombi yao. Naye Nsajigwa alisema kuwa wameamua kuomba radhi wanachama wa Yanga kwa sababu soka ndio kitu wanachokitegemea na kosa walilofanya linaweza kusamehewa.
Wachezaji hao wamesimamishwa miezi sita na klabu yao na kufanya kuondolewa katika kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kinachojiandaa na mashindano ya kombe la Chalenji. Hata hivyo, kuna taarifa kuwa viongozi wa TFF walikuwa wanawahitaji wachezaji hao katika kikosi cha bara na waliwashauri kuomba radhi ili wasamehewe.
NIPASHE
Posted by CM at 8:55 AM
..................................
2 comments:
Anonymous said...
wasamehewe, tuandae timu kwa ajili ya mechi za CAF. Kila mtu ameshajua kosa lake. Hakuna sababu ya kuendelea kug'ang'ania adhabu zisizo na maslahi kwa yeyote.
Dec 6, 2007 4:22:00 AM
Anonymous said...
Nawaomba uongozi Yanga ufikirie msamaha kwa hao wachezaji. Wameshajifunza na nina imani hawatarudia makosa!
-Mosonga
Dec 7, 2007 7:07:00 PM
................................
source: yangatz.blogspot.com
Nilichosema: 30/10/2007
waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa mh. bernand kamilius membe anamkabidhi mizz tz 2007 richa adhia bendera ya taifa katika hafla ya kumuaga iliyofanyika leo kwenye kituo cha uwekezaji, dar. wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji mh. emmanuel ole naiko (shoto) na mkurugenzi wa kamati ya miss tz hashim lundenga
© Michuzi | Tuesday, October 30, 2007
Maoni: 3
............................
Tarehe October 30, 2007 9:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous
Jamani naomba tuandae mjadala wenye Kichwa cha habari:
Bendera yetu ya Taifa inakidhi matakwa ktk mazingira ya sasa?
Wakati wa kupigania uhuru, kujikomboa na kupata uhuru Tanganyika na mapinduzi ya Zanzibar, rangi za bendera yetu zilikuwa na tafsiri yake ktk mazingira ya wakati huo. Lakini sasa mazingira yamebadilika.
Rangi hizo ni:
Kijani- uoto wa asili
Njano-madini na utajiri
nyeusi-wananchi (kwa maana ni weusi??)
bluu-maji bahari, maziwa na mito
Swali langu liko ktk rangi nyeusi ktk mazingira ya leo inawakilisha nini?
Je ni wakati muafaka kubadili au kuongeza rangi ktk bendera ya taifa ili iwakilishe watanzania wa asili (race) tofauti na weusi??
Naomba nieleweke kuwa sina ugomvi na huyu miss TZ ila bendera yetu inamjumuisha? au tuna-assume au kufumba macho na kudhani iko sawa!!
Na Mosonga
source: Michuzi | Tuesday, October 30, 2007
Post a Comment