Saturday, 31 January 2009

Huu ni uzembe!

Kuibiwa kwa mashine ya mionzi ktk Hospitali ya Ocean Road kumesababishwa na watendaji wazembe, achilia mbali walinzi.
Pamoja na kusababisha hasara ya Sh. bilioni moja, maisha ya watanzania wanaohitaji huduma ya mashine hiyo yamewekwa hatarini kutokana na uzembe wa wahusika!
Mambo kama haya yasingepata nafasi kutokea kama umakini ungekuwepo.
Hata hao walioiba mashine nao inabidi wajiulize wanafanya hivyo kwa kumkomoa nani? Kitendo ch wezi hao ni sawa na uuaji maana wagonjwa watakosa huduma muhimu ktk kuokoa maisha hivyo kuweka maisha yao hatarini au hata kuyapoteza.

Tukio hili liwe funzo kwa wahusika Ocean Road na pia hao wezi wazingatie maadili ya kibinadamu na kujali utu wa wenzao.

1 comment:

MOSONGA RAPHAEL said...

Mashine tiba ya kansa yaibwa Ocean Road

Zaidi ya wagonjwa 170 hawatapata matibabu ya saratani (kansa) katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam baada ya mtambo wa kuendeshea mashine za kuchoma mionzi kuibwa hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka taasisi hiyo, kuibiwa kwa kifaa hicho kunafanya shughuli nzima ya uchomaji wa mionzi na tiba ya saratani kusimama.

Akielezea tukio hilo, Mkurugenzi wa Ttaasisi hiyo, Dk Twalib Ngoma, alisema kuwa mtambo huo uliibiwa usiku wa kuamkia jana huku kukiwa na takribani wagonjwa 170 wanaohitaji tiba inayotolewa na mitambo hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Ngoma, mtambo huo hapa nchini upo Ocean Road tu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia watumishi sita kutoka Taasisi hiyo kwa ajili mahojiano zaidi.

Aidha, huduma za tiba ya saratani zitaendelea baada ya kifaa hicho kupatikana au kununuliwa kingine.
Kifaa hicho pamoja na mashine ya mionzi kinagharimu kiasi cha Sh bilioni moja.

SOURCE: Nipashe, 2009-01-31 10:50:32
Na Tamara Manyata