Monday 26 January 2009

Tujali misaada tuipatayo

Napenda kuongelea misaada kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) ya kimataifa ambayo husaidia maendeleo ya wananchi nchini kwetu. Kuna mashirika kama oxfam, worldvision n.k. ambayo tunayo hapa kwetu Tanzania.

Mashirika haya yamekuwa yakiongeza nguvu za maendeleo pale tunapohitaji kupigwa jeki. Na yamekuwa yakifanya hivyo bila kuchoka.

Ni vema sisi tunaofaidika na misaada hii tuonyeshe nia ya kuipokea na kifanyia kazi ipasavyo na kutunza kile wanachotuachia. Hii ni pamoja na matumizi mzuri ya fedha na vifaa tunavyopokea kutoka mashirika hayo. Fedha zitumike katika shughuli zilizokusudiwa na vifaa pia vifanye kazi iliyokusudiwa na kama kuna vyombo vya usafiri tumeachiwa mfano magari, pikipiki, baiskeli n.k. navyo tuheshimu matumizi yake na kuvitunza vidumu.

Haya mashirika yanapata rasilimali na fedha (wanazotuletea) ktk mazingira magumu sana. Hizi ni hela kutoka nchi nyingine ambako wamejinyima wao ili sisi tufaidi, na wakati mwingine hawa watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa hutafuta michango ya wananchi wao kwa njia ya omba-omba -wanasimama mabarabarani na mitaani na kopo au bakuli kuomba mwenye chochote achangie. Kwa kweli wanafanya 'umatonya'ktk nchi zao na wanapopata chochote hutukumbuka ili nasi tufaidi. Wengine hukusanya nguo chakavu (mitumba) na vitabu vya zamani na kuviuza tena ili wapate hela ya kutusaidia.

Kutokana na juhudi za haya mashirika ktk kukusanya chochote ili hela ipatikane kwa ajili yetu wa dunia ya tatu, ni vema nasi tuwe waadilifu ktk kujitolea, kutunza na kuendeleza vitu wanavyotuletea kwa ajili ya maisha na maendeleo yetu. Tuonyeshe kujali na sio kuwakatisha tamaa.

No comments: