Monday, 19 January 2009

Tezzi ni monita la II

Shule za msingi nchini zimefunguliwa juma lililopita 13/01/2009, na watoto wa shule pia wameingia ktk madarasa mapya ndani ya mwaka mpya wa masomo ya shule za msingi.

Mwanangu Tezzi ameingia darasa la Pili mwaka huu, na wiki iliyopita aliteuliwa na mwalimu wa darasa kuwa Monita wa darasa la Pili.

Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mwanangu kufuatia uteuzi wake kushika nafasi hiyo ya umonita. Ameonyesha dalili njema za kiuongozi ktk umri mdogo alionao na ni imani yangu ataendelea kuchipua kipaji alichonacho.

Mimi binafsi na mama yake (kama wazazi wake) tunamtakia kila la heri ktk shughuli zake za kila siku kama mwanafunzi na kiongozi wa darasa (monita). Daima tutaendelea kuwa pamoja nae ktk safari yake hiyo na tutajitahidi kadri ya uwezo wetu ili kuhakikisha anapita ktk njia salama!

Mungu akubariki mwanangu Tezzi.

No comments: