Tuesday, 27 January 2009

Mtoto wa shule azama na kufa maji!

Mwili wa mtoto mmoja mkazi wa mji wa Reading, Uingereza umepatikana jana katika geti moja la mto Kennet na Avon (Fobney Lock) kusini mwa mji (A33 -relief road).
Kijana huyo, 15, alikuwa akiishi maeneo ya Whitley na alikuwa akienda kwa miguu shule iliyoko Southcote (iliyoko mbali kidogo na anapoishi) mnamo tarehe 05/01/2009. Baada ya kutorudi nyumbani, wazazi wake walitoa taarifa polisi na juhudi za kumtafuta zimekuwa zikiendelea kwa muda wa majuma matatu sasa. Hata hivyo juhudi hizo zimekuwa zikikwamishwa na hali mbaya ya hewa.
Inasemekana (kulingana na maelezo ya polisi) kijana huyo wa kiume alikuamua kutumia njia ya mkato kwa kukatisha juu ya mto (uliokuwa umeganda kutokana na kuganda maji na kugeuka barafu) ndipo ajali na umauti ulipomkuta. Au kwa maoni yangu nadhani alitereza kwenye barafu njiani wakati anatembea kando ya mto na kudumbukia kwa bahati . Maji ni ya baridi sana na wataalamu wanasema kuwa hata kama mtu ni muogeleaji mzuri, akidumbukia huko mtoni hawezi kupona maana atazirai kutokana na maji yalivyo baridi na mkondo mkali wa maji.
Mawazo yangu na maombi yapo pamoja na wanafamilia wote wa mtoto huyu hasa wazazi wake ambao walitegemea mtoto wao angepatikana salama badala yake wameletewa taarifa za kupatikana kwa mwili wake uliokuwa umegota ktk lango (lock) la mto kwa muda wa wiki tatu.

No comments: