Tayari baadhi ya watu wameanza kubashiri nini kitatokea mwaka huu 2009.
Jana usiku (22:00 - 01:00 GMT) mtangazaji wa kipindi (Ian Collins) kupitia kituo cha redio cha talksport alitoa ubashiri wake juu matukio makubwa anayotegemea yatajiri ndani ya mwaka huu mpya. Alitoa matukio matatu makubwa:
1. Rais mpya wa Marekani Obama 'atachemsha'. Mtangazaji huyo alitumia maneno 'Obama will disappoint ...' hasa kuhusu utekelezaji wa ahadi alizotoa ktk kampeni.
Hata mimi nadhani Obama hawezi kukidhi matarajio ya wengi. Nimekuwa na wasiwasi huo baada ya kusikiliza ile hotuba yake ya usiku wa kuamkia tarehe 05/11/2008 ya kutoa shukrani kwa wamarekani kwa kumchagua kuwa rais. Ktk hotuba ile Obama alibadilibadili baadhi ya maneno na lugha tofauti na alivyoahidi wakati wa kampeni zake. Kama ukimsikiliza vizuri ile hotuba utagundua amelegeza uzi ktk mambo mbalimbali aliyoahidi.
2. Hakuna uchaguzi mkuu Uingereza. Waziri mkuu, Gordon Brown, ambae ndie mwenye uwezo wa kutangaza uchaguzi mkuu hawezi kufanya hivyo kwa maana anahofia kushindwa ktk uchaguzi na hivyo anaonelea ni bora amalize kabisa muda wake wa kukaa ofisini hadi mwakani.
3. Gazeti moja kubwa litapotea mitaani/madukani. Akalitaja gazeti la 'the independent' kuwa liko ktk hali mbaya kiuchumi hivyo huenda likapotea mwaka huu. Akaongeza kuwa gazeti hilo limekuwa linapungukiwa wateja wa kuweka matangazo ktk gazeti hivyo kuhatarisha usalama wa mapato yake, maana magazeti au vyombo vya habari hutegemea sana matangazo ya biashara ili kujiendesha!
Haya ndiyo mambo ambayo yamebashiriwa kutokea mwaka huu na huyo mtangazaji. Nina wasiwasi kuwa huyo mtangazaji ana mtazamo wa ki-conservative/republican. Kwa hiyo inawezekana mawazo na mtazamo wake ni wa ki-upendeleo (biased), na hivyo mimi binafsi nashindwa kutilia maanani maono yake -kwa maana yanaonekana kuegemea upande mmoja zaidi!.
Friday, 2 January 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment