Tuesday, 14 October 2008

Vitu muhimu Uingereza

Kwa mtu yeyote ambaye ni mhangaikaji (kimaisha) na anaishi Uingereza kuna vitu viwili muhimu ambavyo, aghalabu, ni lazima avifuatilie ktk luninga au redio kabla hajatoka ktk makazi yake kwenda anakotaka kwenda hasa kwa safari ya mbali:
1. utabiri wa hali ya hewa (weather updates)
2. njia za usafiri (traffic news/updates)

Kama mtu akipitiwa au kusahau ku'cheki' hivyo vitu au kimojawapo, anaweza kuonja joto ya jiwe njiani huko aendako! (takuwa kama jusi, joto ya jiwe kwisa juwa!!)
Ni vitu muhimu sana kuvijua karibu kila siku na kila wakati, ndani ya kisiwa cha Uingereza.

No comments: