Tuesday, 7 October 2008

Tuimarishe vikosi vya zimamoto na uokoaji

Napenda kutoa pole kwa familia za wahanga (waliopotez\a maisha na majeruhi) wa ajali iliyotokea Tarime juzi.
Jambo lilonisikisha na uhaba au ukosefu wa vifaa vya uokoaji. Ktk picha nilimwona kamanda Tossi (op maalumu) akiongoza askari wa FFU(?), kwa kweli sikuweza kuwaona au kuwatambua askari wa zimamoto na uokoaji ktk eneo la ajali. Ikumbukwe kuwa ajali ile ilihusha roli la kubeba mafuta na ingewezekana wakati wowote likalipuka na kuongeza maafa zaidi.
Hata hao askari niliowaona kama wa FFU hawakuwa na vifaa kabisa vya kisasa! Walitakiwa wawe na mikasi ya kukatia vyuma ili kuwanasua majeruhi au kuondoa miili ikiwa ktk hali ile iliyoko. Kama mikasi ingetumika kukata dari/paa la basi (kipanya) ingekuwa rahisi kutekeleza zoezi la uokoaji (rescue and recovery). Mikono mitupu kufanya ile kazi nadhani iliwawia vigumu wahusika kukamilisha kazi kwa haraka.

Vifaa vya zimamoto na uokoaji vinaweza kupatikana na kusambazwa ktk wilaya na miji yote nchini iwapo kutakuwa na mipango na mikakati hai ktk ngazi zote, ngazi hasa Taifa (serikali).

Vifaa vya uokoaji ni muhimu ktk maisha na maendeleo ya wananchi, hebu tuchukue hatua madhubuti ili maisha ya raia yasipotee pale yanapoweza kuokolewa. Uzembe na kutokuchukua hatua madhubuti (indecision) kunaweza kusababisha maafa makubwa zaidi.

No comments: