Friday, 17 October 2008

Dedan Karanja Bus

Nimekumbuka mbali sana miaka ya 1980 kule mji wa Musoma, mkoani Mara (Tanzania).

Kulikuwa na basi moja la muundo wa kizamani (enzi hiyo) lililokuwa linasafirisha abiria toka maeneo ya kitongoji cha Makoko, nje kidogo ya mji, hadi mjini Musoma na kurudi tena Makoko. Lilikuwa na mwendo wa taratibu sana! Lilikuwa limeandikwa 'Dedan Karanja' (huenda ni jina la aliyekuwa mmiliki wa basi hilo!)

Kuna basi jingine lililoitwa Mkirya Mwambara (jina la mwenye mali) kwa nyuma lilikuwa na maandishi 'TEREMA BAGAMBE' na dereva wake aliitwa Tondora. Hili basi lilikuwa linasafiri kati ya mjini Musoma na Musoma vijijini kupitia Kiagata (makao makuu ya basi) hadi Baranga, Sirori Simba hadi Ngoreme (Maji Moto). Ni basi lililokuwa linaenda taratibu pia. Terema Bagambe tafsiri yake ni 'Tulia waseme'.

Ktk ruti hiyo ya 'Terema' yalikuwepo mabasi ya mzee Jackson na ndugu yake Muhoni yaliyokuwa na majina 'AHSANTE MWANAMARA'. Nakumbuka jina la kijana wa Jackson aliyekuwa anaendesha moja ya mabasi hayo. Aliitwa Samba. Mara nyingi mabasi haya yalianzia safari zake Sirori Simba, Ngoreme au Masinki (Serengeti) kwenda mjini Musoma. Mzee Muhoni aliwahi kuanzisha ruti ya kutoka Mugumu, Serengeti hadi Musoma mjini na kurudi Mugumu siku hiyo hiyo kwa kupitia Sirori Simba.

Huko ndiko tulikotoka!

No comments: