Hatimaye PCCB kumulika tuhuma hizo na nyimginezo. Hebu tusubiri.
Na Mosonga.
`Sifuati ushauri wa Jaji Bomani`
06 Oct 2007
By Mwandishi Wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bw. Patrick Rutabanzibwa, amesema azma yake ya kumburuza kortini Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, iko pale pale na hatosikiliza ushauri ulitolewa na Jaji Mark Bomani.
Jaji Bomani aliwashauri viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuwa makini kwenda mahakamani kwa sababu Tanzania kuna uhuru wa kuzungumza.
Alisema upo uwezekano, kama hawahusiki na tuhuma za ufisadi, wa kusafisha majina yao bila kupitia mahakamani.
Hata hivyo, Bw. Rutabanzibwa amesema hana haraka ya kufanya hivyo kwa sababu anatafakari kwanza kabla ya kuchukua uamuzi huo huku akishauriana na wanasheria wake.
Alitoa ufafanuzi huo baada ya kuhojiwa na Nipashe iwapo amekubali kufuata ushauri uliotolewa na Jaji Bomani hivi karibuni.
Pamoja na mambo mengine, Jaji Bomani alishauri kuwa, badala ya kwenda mahakamani, ni vyema Taasisi ya Kuchunguza na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iachiwe suala hilo kulichunguza na kuwafikisha mahakamani waliohusika na tuhuma hizo ikilazimika kufanya hivyo ama kuwasafisha.
`Siendi haraka. Natafakari kwanza kabla ya kukimbilia mahakamani na nashauriana na wanasheria wangu na kukusanya ushahidi wa kutosha. Nikijiridhisha kuwa sasa naweza kumpeleka mtuhumiwa mbele ya sheria, nitafanya hivyo,` alisema Bw. Rutabanzibwa.
Alisisitiza kuwa, hakubaliani na ushauri wowote hata kama ni wa kuombwa radhi isipokuwa anachotaka ni kusafishwa jina pamoja na kupata haki yake.
Alifafanua kuwa, licha ya kuwa mambo yanakwenda taratibu, lakini sheria inasema mlalamikaji anaweza kusubiri hata miaka mitatu kabla ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa na atakuwa bado hajachelewa kufanya hivyo.
Alisema, hata hivyo, tuhuma za kumwita fisadi hazieleweki kwani madai dhidi yake yanaelekeza kwamba, alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini kwa muda mrefu (miaka 10) na amehusika katika kuingia mikataba mibovu, mmojawapo ukiwa ni ule wa IPTL.
IPTL ni mradi wa wawekezaji wa Malaysia unaofua umeme wa dharura kwa kutumia mitambo ya dizeli ambao unaigharimu TANESCO Shilingi bilioni tatu kila mwezi, malipo ambayo yanalalamikiwa na Watanzania wengi kwa kubebeshwa mzigo mzito.
Mkataba huo uliandaliwa wakati wa serikali ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassani Mwinyi, una kipengele kisemacho umeme uwe umefuliwa au haujafuliwa, gharama hizo ni lazima zilipwe na ni wa muda wa miaka zaidi ya 10.
Alisema katika madai yake, Dk. Slaa, alitangaza kuwa, kigezo kilichotumiwa kuwaorodhesha mafisadi ni kuangalia namna walivyotumia nyadhifa zao kujinufaisha kwa kuwahujumu Watanzania.
`Hivi kuwa Katibu Mkuu kwa muda mrefu ndiyo kuwa fisadi?
Nitapenda kufahamu namna nilivyotumia wadhifa wangu kujinufaisha katika mikataba hiyo na kuwaumiza Watanzania,` alisisitiza Bw. Rutabanzibwa.
Alisema alitumia dhamana yake kupinga baadhi ya vipengele vya mkataba huo unaolalamikiwa, ambavyo havikuwa na maslahi kwa taifa.
* SOURCE: Nipashe

Saturday, 6 October 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment