Tuesday, 16 October 2007

Asante Mhe Nimrod Mkono (MB)

Natoa pongezi kwa Mhe Mkono (MB) kwa kauli yake alipotembelea Isango!
Na Mosonga

Shule aliyosoma Waziri
Sitta yageuka kichaka
Ilifungwa na Profesa Kapuya
NA EVA SWEET MUSIBA, MUSOMA
SHULE ya Sekondari ya Isango, wilayani Rorya, Mara, aliyosoma Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta, imefungwa kwa kipindi kirefu, hivyo kugeuka kuwa kichaka na makazi ya popo.
Kwa mujibu wa taarifa, shule hiyo ilifungwa mwaka 1997 na aliyekuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, Profesa Juma Kapuya, kwa maelezo kwamba ni chakavu na haina samani. Profesa Kapuya kwa sasa ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono aliitembelea shule hiyo hivi karibuni, akiwa amefuatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere. Shule hiyo ni mali ya Jumuia ya Wazazi ya CCM.
Mkono alisema amesikitishwa na kitendo cha kufunga kwa shule hiyo na kuachwa kuwa gofu.
Licha ya kufungwa, baadhi ya walimu bado wanaishi katika maeneo ya shule hiyo, huku wakiendelea kutumia ofisi zilizo chafu na chakavu.
Mkono akizungumza na baadhi ya walimu hao, alisema anataka kuona shule hiyo inafunguliwa, na kama watahitaji msaada yuko tayari kutoa.
Akiwa shuleni hapo, pia alikutana na ofisa miliki wa mali za jumuia hiyo ya Chama, Kapteni mstaafu Mohamed Ligora, ambaye alikwenda kukagua shule hiyo.
Mkono alionyesha kushangazwa na hali ya shule hiyo, akisema watoto wanakosa elimu, wakati shule ipo kinachotakiwa ni kuikarabati.

source: Uhuru

No comments: