Tuesday, 9 December 2008

Uhuru wa Tanganyika: Miaka 47 leo

09/12/2008
Leo ni siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara).
Naitakia kila la heri nchi yangu Tanzania. Tanzania Bara ilipata uhuru wake tarehe 09/12/1961.

Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo woteee!
....
Nilalapo nakuota wewe, jina lako ni tamu sana wee!
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
.

(Nilipokuwa JKT Masange, mwaka 1990, Mkuu wa JKT wakati huo Maj.Gen. Makame Rashid alitoa ofa ya 'pass' ya siku 3 ikiwa kuruta (serviceman/woman) atajitokeza na kuuimba wimbo huu wote! Dada mmoja alipata pass hiyo!
Maj. Gen. Makame alikuwa ametembelea kambi yetu iliyokuwa jirani na Kalunde, jimbo la Tabora Kaskazini)

No comments: