Thursday, 11 September 2008

Usafiri wa bure kwa wazee wetu

Nimeona mfano mzuri Uingereza kuwa raia wao waliostaafu au wenye umri kuanzia miaka 65 wanapewa kadi (pass) ya kusafiri bure maeneo anayoishi (local ares) ktk vyombo vya usafiri vya umma (public) mfano mabasi, treni n.k. Wana mpango wa kupanua huduma hii ili wazee hawa wasafiri nchi nzima popote watakapo. Mpango huu hulipiwa na halmashauri za serikali za mitaa na serikali kuu hutoa fungu kidogo.

Pia ktk matamasha na burudani nchini Uingereza, viingilio ktk mechi za mpira au kumbi za burudani za mbalimbali wazee (senior citizens) hulipa viingilio nusu (concessions) sawa na vya watoto.

Kwetu Tanzania nako tunaweza kusaidia watu wenye umri mkubwa kusafiri bure au hata kwa nauli nusu ya mtu mzima. Serikali za mitaa na serikali kuu inaweza kutafuta namna ya kulipia huduma hizi.

Natumaini iko siku wazee wetu watapata ahueni ktk maisha yao ya uzeeni, wamechangia nguvu zao tangu wakiwa vijana na sasa wanahitaji kufaidi jasho lao walilolimbikiza wakilitumikia Taifa ktk nyanja mbalimbali walizozipitia kimaisha iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri, kote huko waliweza kulipa kodi. Huu ni wakati wao sehemu ya kodi zao ziweze kuwatunza!

No comments: