Monday, 1 September 2008

Mfuko wa Mwalimu Nyerere wapigwa jeki

Kaimu Katibu Tawala wa MNF, Gallus Abedi, amesema Mfuko wa Mwalimu Nyerere umepokea michango ya fedha na vitu mbalimbali kutoka kwa watu maarufu duniani, akiwamo Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Waziri Mkuu wa India, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.

Waliotoa michango hiyo ni Waziri Mkuu wa India: kompyuta tano na mashine zake, zenye thamani ya Sh. 8,482,000.

Wengine waliochangia ni taasisi ya Anglo-American Prospecting Services Ltd na michango iliyofanyika katika mikoa kadhaa nchini.

Nelson Mandela alichangia dola 608,000 (Sh. 405,015,916.80).

Wengine, ni Gaddafi: dola 200,000 (sh.177,800,000), Kagame: dola 200,000 (sh. 172,500,000), Museveni: milioni 1 (sh. 910,954,160), JWTZ: sh. 51,576,600 na michango iliyofanyika mikoa kadhaa nchini: sh. 512,857,030.
-source: Nipashe, 01/09/2008

No comments: