Tuesday, 9 September 2008

Familia na Ushauri Nasaha

Wapo watu wengi ambao hudhania kuwa ushauri nasaha unatoka kwa wataalamu fulani tu!
Mimi nafikiri kuwa mtaalamu bingwa wa mambo ya ushauri nasaha kimaisha ni familia husika ya mtu mwenye hitaji fulani (au tatizo) maana ndio wanaomjua mtu husika kwa vile wamekua pamoja tangu udogoni au wanatumia muda mrafu na hivyo ni rahisi mmoja wa familia kusaidia mwenzake.

Kitu kingine. Wapo tena watu wengi ambao hudhani msaada kwa mtu ni lazima uwe wa kifedha au kitu fulani. Kwa mara nyingine mimi naelewa ktk namna tofauti juu ya hili.
Kwangu mimi naamini msaada mkubwa kabisa na usionunulika kwa bei yoyote ni msaada wa kimawazo, maoni na ushauri. Wengi wanapokaribiwa na mtu akihitaji msaada wa mawazo mara moja hudhani kuwa hiyo ni 'gia' ya kuomba kitu fulani - kumbe sio.

No comments: