source: majira, 28.03.2008 0856 EAT
Na Peter Mwenda
MVUA za masika zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam zimesababisha vifo vya watu wanne kwa kuangukiwa ukuta na wengine kufa maji.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Bibi Rukia Simbakalia, alisema jana kuwa katika tukio la kwanza, Bw. Said Mkubwa (75), alikufa baada ya kuangukiwa na ukuta nyumbani kwa mwanawe, Bw. Fadhili Lila (32) wa Mbagala Kiburugwa.
Nae Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow, alisema katika tukio lingine, Khadija Shaaban (3) alikufa baada ya kuangukiwa na ukuta wa choo wakati akijisaidia pembeni mwa ukuta huo eneo la Manzese Uzuri.
Alisema mwili wa mtoto wa mwaka mmoja, Rehema Hamisi, ulikutwa ukielea kwenye mfereji uliojaa maji yaliyotokana na mvua kubwa kunyesha juzi katika mkoa wa Dar es Salaam.
Kamanda Rwambow alisema maiti hao wamehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.
Friday, 28 March 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment