Thursday 20 March 2008

Kamati za Bunge: Viongozi na Wajumbe

WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekutana Dar es Salaam kuchagua wenyeviti wa kamati mpya za Bunge ambapo wabunge machachari wa kambi ya upinzani na chama tawala, wameibuka washindi katika uenyekiti na unaibu wa kamati nyeti.

Kamati mpya ya Hesabu za Mashirika ya Umma:
Mwenyekiti - Bw. Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini, CHADEMA) na
Makamu M/kiti ni Bibi Estherina Kilasi (Mbunge wa Mbarali, CCM).

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa:
Mwenyekiti- Dkt. Wilbroad Slaa (Mbunge wa Karatu, CHADEMA) -alipita bila kupingwa Makamu M/kiti- Bw. Mgana Msindai (Mbunge wa Iramba Mashariki, CCM)


Kamati ya Hesabu za Serikali,
Mwenyekiti- Bw. John Cheyo (Mbunge wa Bariadi Mashariki, UDP)
Makamu M/kiti- Bw. Zubeir Ali Maulid (Mbunge wa Kwamtipura, CCM).

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge:
Mwenyekiti- Bibi Anne Malecela (Mbunge wa Same Mashariki, CCM)
Makamu M/kiti- Bw. Abdulkarim Shah (Mbunge wa Mafia, CCM).


Kamati ya Miundombinu:
Mwenyekiti-
Makamu Mwenyekiti- Bibi Anne Malecela (Mbunge wa Same Mashariki, CCM)

Kamati ya Nishati na Madini:
Mwenyekiti- Bw. William Shelukindo (Mbunge wa Bumbuli, CCM)
Makamu m/kiti- Dkt. Harrison Mwakyembe (Mbunge wa Kyela, CCM)

Kamati ya Fedha na Uchumi:
Mwenyekiti- Dkt. Abdallah Kigoda (Mbunge wa Handeni, CCM)
Makamu M/kiti- Bw. Hamza Mwenegoha (Mbunge wa Morogoro Kusini, CCM)

Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama:
Mwenyekiti- Bw. Wilson Masilingi (Mbunge wa Muleba Kusini, CCM)
Makamu M/kiti- Bw. Azzan Zungu (Mbunge wa Ilala, CCM)
Mbunge wa Monduli (CCM), Bw. Edward Lowassa alichaguliwa kuwa mjumbe.

Katika tukio lingine Mbunge wa Viti Maalumu, Bibi Lucy Owenya (CHADEMA) alilalamikia hatua ya kupangwa katika Kamati ya Viwanda na Biashara akiwa mpinzani peke yake huku kamati hiyo ikiwa na vigogo wengi kutoka chama tawala.

Mbunge huyo alitaja vigogo hao wa CCM ambao alidai kuwa watamzidi nguvu katika kamati hiyo kuwa ni Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Bw. Nazir Karamagi, Mbunge wa Makunduchi, Bw. Abdisalaam Issa Khatib, Mbunge wa Tanga, Bw. Bakari Mwapachu, Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Bw. Joseph Mungai na Mbunge wa Rombo, Bw. Basil Mramba.

Bibi Owenya alisema atafikisha malalamiko hayo kwa Spika, Bw. Samwel Sitta, ili kamati hiyo iongezwe mbunge mwingine kutoka kambi ya upinzani watakayesaidiana naye.

Kamati ya Nishati na Madini chini ya Bw. Shelukindo na Dkt. Mwakyembe, inatarajiwa kuanza kazi leo Dar es Salaam kwa kusimamia semina ya wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya Petroli na Umeme, ambayo ilivunjika wakati wa mkutano wa Bunge uliopita mjini Dodoma, baada ya wabunge kudai kupewa kwanza ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyochunguza kashfa ya kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond.


source: majira, 19.03.2008 0145 EAT
Na Joseph Lugendo

Note: (I have omitted some "flesh" of the original story to make it short)

No comments: