Tuesday, 24 February 2009

Umaskini wa Nishati

Pamoja na kwamba nchi kama Uingereza imeendelea na iko ktk dunia ya kwanza wapo wanachi wa nchi hiyo ambao wanaishi ktk aina 'mpya' ya umaskini.

Wananchi walio ktk tabaka la kati na chini kiuchumi wako njia panda kiuchumi kutokana na ugumu wa maisha na hasahasa kutokana na bei za kulipia bili mbalimbali kupaa hewani!

Kipato wananchopata hakitoshi kukidhi mahitaji yao ya kawaida ya kila siku. Mshahara ukipatikana bili ya kwanza kabisa kulipwa ni deni la nyumba (mortgage) au pango (house rent). Malipo ya bili hii ndiyo makubwa kuliko yote! Baada ya hapo bili ya umeme, gesi na maji hufuata (maana bila kupasha nyumba joto mtu unaweza kukauka kwa baridi ktk kipindi hiki cha baridi (winter). Baadae bili ya chakula!

Lakini kutokana na makali ya maisha mtu anaweza akaamua kutolipia bili ya umeme/gesi ili anunue chakula kwa ajili ya familia. Hali hii inajulikana kama umasikini wa nishati - kwa kimombo wanaita 'fuel poverty' - kwa maana watu hujiuliza 'should we EAT or HEAT?

No comments: