Kikosi cha Polisi cha Thames Valley kimetangaza kuwatafuta raia wema wa Uingereza (wa kujitolea)watakaopenda kujiandikisha ili wawe wapelelezi wa polisi kwa ajili ya kuwachunguza polisi! Imeeleweka hiyo?
Hii ni staili ya wale watu wanaoitwa huku kama 'mystery shoppers'. Watu hawa huingia dukani au ofisini na kujifanya wateja lakini lengo lao kuu ni kuchunguza kama wahudumu husika wanawajali wateja na kuzingatia miiko ya kazi. Watu hawa huripoti kwa wakubwa wa maduka au ofisi husika. Lengo la kuwatumia 'mystery shoppers' ni kuboresha huduma kwa wateja na kulinda heshima ya wenye duka au ofisi hasa ktk kipindi hiki cha dunia ya ushindani.
Kwa hiyo hao raia wakijitokeza wataandikishwa kibarua (cha kujitolea) na polisi kwa siri. Kazi yao ni kujifanya kama wamepatwa na matatizo fulani (victims) mfano kubakwa, kuibiwa au tatizo lolote. Kisha wanaripoti polisi. Hapo ndipo kazi yao itaanzia, kazi yao hasa itakuwa kutathmini jisi polisi walivyoshughulikia tatizo lao na kisha kuripoti kwa siri kwa wakubwa wa polisi. Ni kama kuwachunguza utendaji wa polisi kimtego!
Kazi kwao hao mapolisi watakaochemsha au kuzembea kazini, Big Brother Huyo kaingia! Kaeni chonjo, hii ni saa mbaya!
Je huko kwetu TZ uwajibikaji uko ktk kiwango gani. Wenzetu wanatafuta namna ya kusafisha jeshi ni vizuri na sisi tujiangalia nafasi yetu.
Friday, 13 February 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment