Saturday, 24 May 2008

Tibaigana: Mfano wa kuigwa kimaisha!

Mzee Alfred Tibaigana kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam anatarajia kustaafu mwezi wa saba mwaka huu.
Nimefurahi kuona mawazo yake na mipango aliyojipangia kimaisha baada ya kustaafu. Kwa kweli ni mfano wa kuigwa!
Kilichonifurahisha zaidi ni uamuzi wake wa kujianzishia miradi mbalimbali ili aweze kujiajiri kupitia miradi ya kilimo na biashara.
Watanzania tulio wengi huwa tunafikiria kuwa hakuna ajira nchini na hivyo tunajikalia kitako mchana na usiku huku tukilaumu ugumu wa maisha!
Mzee Tibaigana ametufungua macho kuwa inawezekana kujikimu kimaisha endapo tutaamua kutumia rasilimali zilizopo kama vile ardhi na nguvu zetu wenyewe kuweza kujiingizia kipato kimaisha.
-mosonga2002@yahoo.com
...........................................
............................................
soma mikakati ya kimaisha ya mzee Tibaigana hapo chini!
..........................................
Mbali na nia hiyo ya kugombea ubunge, Tibaigana alisema kuwa atakapostaafu atajihusisha na biashara ya kuendesha hoteli ambayo ameshaijenga pamoja na wenzake eneo la Mkuranga mkoani Pwani. Kwa mujibu wake, Mkuranga pia ana shamba la mananasi, mapasheni na anafuga nguruwe, mbuzi, ng’ombe na kondoo.

Pia kijijini kwao katika Kata ya Buganguzi, wilayani Muleba ana shamba la migomba na anafuga ng’ombe. Wakati anaondoka katika nafasi hiyo ya ukamanda wa Dar es Salaam, Tibaigana mbali na kuwashukuru wakazi kwa ushirikiano waliompa katika kazi, ametoa mwito waheshimu sheria kupunguza ajali.

No comments: