Friday, 6 July 2007

Kandanda Tanzania: Ligi ya miezi 3!

Ninashangaa kwamba taifa letu ni kubwa kieneo na idadi kubwa ya watu lakini tuna ligi ya mpira wa mguu ya miezi 3! Nakumbuka ligi imeanza mwezi Machi mwaka huu, na leo hii nasikia fainali ni Yanga na Simba!
Hii ligi haikuwa ya ushindani kabisa. Wachezaji ambao wanategemea mpira kama ajira hasa kwa timu zisizoingia sita bora wanaishije ktk kipindi cha miezi 9 ikiwa ligi iko hai miezi 2 -3 tu! Likizo gani ndefu kiasi hicho, na je wachezaji wanaowakilisha taifa wanapataje maendeleo endapo timu zao haziko ktk ligi kwa kipindi chote hicho?
Nina wasiwasi na kiwango cha soka nchini kwamba kinadumaa badala ya kukua maana mchezaji hawezi kukaa bure bila mashinadano halafu ukategemea atatunza kiwango chake au kukiendeleza.
Tutaendelea kweli?

No comments: