Tuesday, 4 November 2008

Piga kura yako sasa hivi ili Obama ashinde!

Kwa wale wapiga kura wa Marekani leo ndio siku ya kufanya kweli.

Muda wa kampeni na longolongo umekwisha kabisa. Sasa ni saa ya hukumu.

Tumia kura yako kumpa Seneta Obama ushindi. Seneta Obama hawezi kuwa Rais kwa maneno matupu bali kwa kura yako!

Enyi wapiga kura wa Marekani, mashabiki na wapenzi wa Seneta Obama, amkeni sasa hivi, bila kupoteza wakati, nendeni moja kwa moja kituo cha kupigia kura mkampigie kura Seneta Obama.

Najua wengi wenu mtakuwa mmketi kwenye sofa huku macho yenu yameganda kwenye luninga (TV), mkifuatilia 'exit polls' za wenzenu wakati hata nyie mnatakiwa mkapige kura!

Usitegemee Seneta Obama atashinda kwa kura za wapiga kura wengine. Ukweli ni kwamba Seneta Obama atashinda kwa kura YAKO WEWE, yule na wale! Timizeni wajibu wenu kwa umoja.

If you don't vote now, NO victory for him.

Every vote counts.

So, get up and vote for Sen. Obama, NOW!!!

No comments: