Dondoo nyingine muhimu kuhusu EPA ni kama ifuatavyo:-
Benki zilikopitishwa fedha
Bank of Baroda (T) LTD,Barclays, CRDB, Diamond Trust, Eurafrica, Exim Bank, Kenya Commercial Bank, NBC, Standard Chartered na United Bank of Afrca.
Vigogo BoT walioidhinisha
Vigogo hawa walioshika nyadhifa hizi au kuzikaimu katika kipindi cha kuchotwa fedha hizo, ni miongoni mwa watuhumiwa: Gavana wa Benki Kuu (hayati Dkt. Daud Ballali), Mkurugenzi wa Fedha, Katibu wa Benki Kuu (wako wawili) na Mkurugenzi wa Sera za Uchumi (wako wawili).
Wengine ni Naibu Mkurugenzi Idara ya Madeni (wako wawili), Mkuu wa Kitengo cha Madeni ya Biashara, Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Benki na Bodi ya Wakurugenzi iliyokuwepo mwaka 2005/2006.
Kampuni 'zilithibitika' kughushi
Kampuni hizi zilithibitika kuwa ziliwasilisha nyaraka feki katika kuchota fedha kwenye EPA nazo ni Bencon International of Tanzania, VB and Associates of Tanzania, Bima Resorts, Venus Hotel, Njake Hotels and Tours, Mahan Mining company of Tanzania na Money Planners and Consultants.
Nyingine ni Bora Hotels and Apartments, B.V Holdings LTD, Ndovu Soaps, Navy Cut Tobacco LTD, Changanyikeni Residential Complex na Kagoda Agriculture LTD.
Utata kampuni 9
Kampuni tisa zifuatazo ziliwasilisha nyaraka ambazo badohaijathibitika kama ni feki au halali kutokana na kampuni za nje zinazodaiwa kuwaruhusu kupokea malipo kwa niaba yao kila wanapoulizwa kukaa kimya mpaka sasa.
Kampuni hizo ni G&T International, Excellent Servies LTD, Mbale Farm, Liquidity Serives LTD, Clayton Marketing LTD, M/S Lashlas (T) Limited, Malegesi Law Chambers Advocates, Kiloloma and Brothers na KERNEL LTD.
Mapendekezo ya wakaguzi
*Ufanyike uchunguzi kamili wa kijinani dhidi ya makampuni hayo na maofisa wa BoT kisha zichukuliwe hatua kali.
*Uanzishwe utaratibu wa kisheria wa kuhakikisha fedha zinarejeshwa.
*Hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wa BoT waliosaidia kuchotwa fedha hizo.
*Yafanyike mawasiliano na kampuni za nje zinazodaiwa kutoa idhini ili ijulikane ukweli kuhusu zile kampuni tisa ambazo malipo yao yanayofikia sh. bilioni 42.
*Uanzishwe mkataba wa muongozo kati ya Wizara ya Fedha na BoT juu ya uendeshaji wa akaunti ya EPA ili kuwe na:-utaratibu wa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya akaunti, hali ya madeni na dhamana zote ziwe zinaidhinishwa na Wizara.
*Ili kupambana na usanii, BoT na Serikali ziangalie ushauri wa kisheria ili siku nyingine zikatae kujihusisha na 'watu wa tatu,' katika ulipaji wa madeni, badala yake kampuni zinazodai zije zenyewe.
*Chanzo:Ripoti ya ukaguzi ya Ernst and Young iliyotolewa Januari, 2008. (kutoka: gazeti majira, 03/11/2008)
Monday, 3 November 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment