Thursday, 31 January 2008

Mkoa wa Pwani

Sio kawaida majina ya watu au mahali fulani (miji) kutafsiriwa ktk lugha nyingine.
Kwa mfano kama mtu anaitwa B Maji, litabaki hivyo hivyo hata kama limetumika ktk chombo cha habari kinachotumia lugha ya kiingereza na sio B Water! Hali kadhalika jina la mji kama Mto wa Mbu litakuwa hivyo hivyo na sio River of Mosquites!!
Mifano mingine ni Cha Cha Mapinduzi (CCM), Chadema, TLP huwa havitafsiriwi ktk lugha nyingine vinabaki na majina yao ya asili.
Isipokuwa kwa mkoa wa Pwani (Tanzania) inanishangaza huwa unabadilika kulingana na lugha inayotumika. Kwa kiswahili unaandikwa au kuitwa Pwani wakati lugha ya kiingereza inapotumika utaona mkoa wa Pwani unaandikwa au kuitwa 'Coast' region!
Kwangu mimi naona sio sahihi. Au labda ni sahihi siwezi kujua!!

No comments: