Ktk maisha daima angalia mbele, zingatia nafasi na uwezo wako. Kile unachoweza kifanye na kisichowezekana kwako kiache usiwe mshika mbili. Ridhika na ulichobarikiwa nacho, acha kutamani kisicho riziki.
Kumbuka 'happiness is not having what you want but wanting what you have' (msemo wa kizungu)!
Pia wa kale walisema, 'moyo wangu sultani cha mtu sikitamani'.
Matatizo yasikuyumbishe ukapoteza dira bali yawe chachu ya kukupa moyo na matumaini. Bila shaka utashinda kwa mapenzi na nguvu za Muumba wetu!
Saturday, 26 January 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment