Tuesday, 19 January 2010

Mtoto na elimu

Mara nyingi huwa nasisitiza kwa watoto mashuleni kujitahidi kupata alama za juu ktk mitihani badala ya kukazania mtoto kuwa wa kwanza!

Hakuna ubaya wowote kama mtoto atapata wastani wa alama 80 kwa mia au zaidi na akawa wa 15 darasani! Kuwa wa kwanza sio kitu cha ulazima au kigezo cha uelewa, cha muhimu ni 'performance' na 'progress' ktk masomo darasani iwe ya kuridhisha!

Kumbuka mtoto anaweza kuwa wa kwanza darasani kwa, mathalani, alama za 40 hadi 50 kwa mia kwa vile tu amewazidi wenzie darasani, lakini kwa kipimo halisi alama alizopata mtoto huyu ni za chini sana na pia kiwango chake hakiridhishi! Na mara nyingi watoto wa kundi hili huwa hawana ushindani wa kutosha madarasani mwao!

Hata hivyo, itapendeza zaidi endapo mtoto atapata maksi za juu na pia akawa wa kwanza darasani!


Nawatakia mafanikio mema watoto wote wenye bidii ktk masomo. Nawahimiza kuwa waendelee kuwa wadadisi masomoni na kwa hakika watafanikiwa kitaaluma na maisha kwa ujumla.

Elimu ndio msingi wa maendeleo!!!

No comments: