Thursday, April 02, 2009
Rais wa Marekani Barack Obama jana aliwaacha hoi waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali hapa Uingereza hasa BBC tv na Sky News ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu nje ya makazi ya balozi wa Marekani jijini London.
Rais Obama alikuwa anategemewa kuondoka kutoka ktk makazi hayo ya balozi kabla ya saa 2 za asubuhi kwa saa za Uingereza. Nilikuwa naangalia habari kupitia BBC One, kipindi cha Breakfast, ambapo mtangazaji Billy Turnbull alisema wanakatisha ratiba za kawaida ili kumsubiri Rais atoke akielekea ofisi ya Waziri Mkuu Gordon Blair. Zaidi ya robo saa ilipita huku watazamaji wakimsubiri Rais na msafara wake! Kamera zote zilikuwa zinamulika 'live' geti atakalotokea Rais.
Ghafla bin vu, kamera nyingine za BBC zikaonyesha msafara wa Rais umekaribia geti la Downing Street -makazi na ofisi ya Waziri Mkuu! Alikotokea Rais bado haijulikani na watangazaji walibaki hoi!
Kumbe Obama nae ni komandoo!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment