Tuesday, 26 August 2008

Kinyesi cha ng'ombe

Sio rahisi kufikiria kuwa Ulaya unaweza kupuliziwa na harufu kali za kinyesi cha mifugo. Juzi juzi nikiwa njiani eneo la Shiplake, Oxon (Uingereza) nilipigwa na harufu kali sana ya kinyesi cha ng'ombe huku gesi ya amonia ikitumbuiza kwa mbali. Nilipopiga jicho niliona mifugo aina ya ng'ombe wa kisasa wakiwa wanachunga nje (kwa vile huu ni wakati wa summer).

Leo tena bila kutegemea maeneo ya Yateley, Hants nimesikia jogoo wakiwika zaidi ya mara mbili, nilihisi niko kijijini kwetu TZ!!

Kumbe maisha ni yaleyale tu si Ulaya si TZ, wazungu wanatuzidi kidogo tu hasa kwa jinsi wanavyotumia rasilimali zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Watanzania tungelikuwa mbali na sisi kama tusingelikuwa wadokozi wa 'vijisenti' hapa na pale!

No comments: