Hivi karibuni (miezi kadhaa hivi iliyopita) nilienda Mwanjelwa jijini Mbeya kutafuta/kununua tv. Baada ya kupitapita nikafika duka moja na nikaipenda tv moja aina ya hitachi. nikaomba waniletee mpya (siyo ya display window). Jamaa mwenye duka akaleta moja ya hitachi. Tatizo likawa hiyo tv iko ktk box la tv aina ya Ouling(?) -made in China na remote yake haikuwa na nembo/brand ya hitachi. Nikaikataa tv na kuondoka!
Kesho yake nikaamkia mji wa Tunduma mpakani na Zambia. Nikaingia duka moja linaloaminika mji mzima. Baada ya kupitisha macho huku na huko nikapendezewa na tv aina ya philips. Nikaiagiza waniletee. Nikasubiri wakaichukue 'stoo' na baada ya kama nusu saa baadae ndo mtu akaibuka nayo!
1. ilikuwa ktk box la tv aina ya ouling - made in China!!!
2. ikawekwa mezani - testing time (nayo pia ilikuwa na nembo 'pure' ya philips). alipoiwasha tu ile rangi ya bluu ikatokea ikiwa imebeba jina la 'HITACHI'!!!!
3. baada ya kuuliza kulikoni philips inaandika hitachi ktk kioo wakajibu: ukitaka tunaweza kukubadilishia nembo na kukuwekea ya hitachi ifanane na hayo maneno.
Kumbe tv huwa zinaingizwa hazina majina yaliyobandikwe pale mbele, ila maneno hayo nayo huagizwa separately (kwa magendo)na kuja kuwabambika watu Bongo!
Kumbe kule kuchelewa kote kuleta tv walikuwa wanagundisha kialama cha philips kwenye tv maana hata gundi ya superglue ilikuwa inaonekana kama ukichunguza pale kwenye jina la tv na pia walikuwa wamepindisha kidogo maandishi hayakuwa ktk mstari sambamba!
hii ndio Bongo Bandugu! Usidhani tv mpya unayonunua ni brand kamili uliyokuwa unaifikiria (kama umenunua tv mpya Bongo).
ABIRIA CHUNGA MIZIGO YAKO! MALI IKISHANUNULIWA HAIRUDISHWI!
..............................................................
Thursday, 29 July 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment