Monday, 2 November 2009

Kondomu za familia

Angalau sasa watu wazima tumepata pa kupumlia baada ya watu fulani kupata 'aidia' poa ya kiutu uzima!!!

Awali au zamani kidogo mtu kuagiza kondomu dukani ilikuwa ni kibarua pevu hasa umkutapo mtu wa makamo au wa jinsia tofauti!!! Utaanzaje kusema au kuuliza ni kondomu gani nzuri au imara? (maana kondomu nayo ni bidhaa kama nyinginezo - maana waweza uliza sabuni gani nzuri kati ya foma na omo?). Je ktk kondomu waweza muuliza muuzaji ni zipi nzuri kati ya salama na dume? La hasha, zamani haikuwa rahisi!

Siku hizi zimeingia kondomu za kiheshima kabisa - maalumu kwa waliooana (mambo ya uzazi wa mpango!) Zinaitwa 'Familia Kondomu'.

Kwa wale wakware (wazinzi) wamepata kisingizio. Mtu una 'appointment' (miadi) na 'totoz' unaenda kununua 'familia kondomu hata hapo duka jirani - hakuna wa kukuhisia vibaya (si una mke! hata kama zaenda nyumba ndogo nani atastukia?).

Kwa waliooana mambo ni shwari siku hizi (naongelea wasio waaminifu). Hata kama kondomu zitaonekana mifukoni au mikobani, mwenzio hawezi kuhisi vibaya maana inaonyesha unazingatia uzazi wa mpango, ingawa pia hawezi kujua zilikuwa ngapi wakati zinanunuliwa na zimefika nyumbani ngapi!!

Yaani unanunua kwa kujiamini popote wakati wowote kwa kivuli cha uzazi wa mpango na hata kuzihifadhi hakuna wasiwasi ila pa kuzitumia 'part-time' ni siri ya mhusika!

Je, waliozibuni hizi kondomu za familia lengo kuu walifikiria kuokoa maisha ya watu (kwa wale waonao aibu kununua dukani - kwa woga wa kuonekana ni mafuska?) Maana kama ni mambo ya uzazi wa mpango, mbona kondomu zilikuwepo tangu zamani na zinafaa kwa kazi hiyo?

No comments: