Thursday, 4 June 2009

Watoto wa teknolojia

Juni IV, MMIX
Jana nilipokea ujumbe wa maneno kwa simu ya mkononi kutoka kwa mwanangu ambaye ameanza masomo ya shule ya msingi hivi karibuni. Nilishangaa sana.

Siku hizi watoto wadogo kabisa nchini wanaweza kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa, mfano kompyuta, simu za mkononi n.k. bila shida. Bila shaka haya ni maendeleo ya kutia moyo.

Sio muda mrefu ujao, suala la ujinga litakuwa sio kutojua kuandika na kusoma bali kutojua kutumia kompyuta. Na hii ndio itakuwa vita mpya kitaifa! Miaka ya 1970, Mwalimu aliendesha kampeni ya 'Jifunze Kusoma, Wakati ni Huu'. Mimi nadhani huu ni wakati wa kuzindua kampeni mpya ya kujifunza kutumia 'teknolojia ya habari' ya kisasa.

Ikumbukwe kuwa kizazi cha watu wazima wa sasa wameanzia ukubwani kuziona na kuzitumia teknolojia hizi!

No comments: