tag:blogger.com,1999:blog-1405840685412848847.post1044169521170575884..comments2023-12-17T20:07:35.752+00:00Comments on OPEN HEART, OPEN MIND: Tabia ya mtuMOSONGA RAPHAELhttp://www.blogger.com/profile/11344559339311484137noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-1405840685412848847.post-19653300841901135372008-09-11T11:11:00.000+01:002008-09-11T11:11:00.000+01:00Ghorofa jingine la Wamachinga kujengwa Manispaa ya...Ghorofa jingine la Wamachinga kujengwa Manispaa ya Temeke

2008-09-10 17:22:29
Na Sharon Sauwa, Temeke

Halamashauri ya Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es Salaam imetoa notisi ya kutoendelezwa kwa maeneo waliyopewa katika soko la TAZARA Vetenary ili kupisha ujenzi wa Jengo la kisasa la wamachinga.

Meya wa Manispaa ya Temeke, Bw. Jerome Bwanausi, ameliambia Alasiri kuwa wafanyabiashara hao kuwa hivi sasa, tayari Manispaa hiyo imeshaanza kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.

Hata hivyo, akasema bado haijafahamika jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara wangapi na gharama za ujenzi wake zikoje.

Akasema wawekezaji kutoka China wameonyesha nia ya kuingia ubia katika ujenzi wa jengo hilo.

"Tayari Halmashauri ya Temeke imeshatoa notisi kwa wafanyabiashara kutoendeleza maeneo hayo kwa ajili ya kujenga jengo hilo,"akasema Bw. Bwanausi na kuongeza kuwa wawekezaji hao kutoka China wamefika katika eneo hilo na kuliangalia.

Akasema wafanyabiashara ambao watatoka katika eneo hilo watapata nafasi katika jengo la wamachinga linalojengwa Kariakoo na kwamba wale watakaokosa nafasi watapewa kipaumbele katika jengo hilo la Tazara litakapokamilika.

Akasema utaratibu unaandaliwa kwa ajili ya kuwapatia nafasi katika jengo la Kariakoo, ili waweze kuachia nafasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo hilo.

Hivi karibuni kundi la wafanyabiashara 68 kutoka katika soko hilo walielezea kuhusiana na kusimamishiwa kwa ujenzi wa vibanda vya biashara Tazara Vetenary.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Bw. Musa Kitenga, alisema waliiomba manispaa iyo iwapatie nafasi katika soko hilo kwa kipindi kirefu bila kujibiwa na hivyo kulazimika kumuona Diwani wa kata ya Chang'ombe, Bw. Noel Kipangule, ambaye aliuamuru uongozi wa soko kuwapatia nafasi.

Hata hivyo, akasema wakiwa katika ujenzi uongozi wa manispaa ulifika na kuwakataza kuendelea na ujenzi kwasababu diwani hakuwashirikisha katika maamuzi.

Akaiomba Serikali kuwapatia nafasi ya kufanyia biashara ili waweze kufanya shughuli zao na kuweza kujikimu kimaisha.

SOURCE: AlasiriMOSONGA RAPHAELhttps://www.blogger.com/profile/11344559339311484137noreply@blogger.com